Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Masheikh Uamsho walipwe fidia
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Masheikh Uamsho walipwe fidia

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

MWENYEITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameiomba Serikali iwalipe fidia viongozi 18 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), waliofutiwa mashtaka ya ugaidi, baada ya kusota rumande miaka nane. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Masheikh hao wa Uamsho, walifutiwa mashtaka ya ugaidi katika Kesi ya Jinai Na. 121/2021, iliyokuwa inawakabili pamoja na Masheikh wengine 18, kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, tarehe 15 Juni 2021 na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu.

Akizungumza katika ziara yake kwenye Kanda ya Kusini, jana tarehe 16 Juni 2021, mkoani Mtwara, Mbowe alisema Masheikh hao wanastahili fidia, kufuatia athari walizopata wao na familia zao, walipokuwa mahabusu gerezani tangu 2012.

“Je, hasara iliyopatikana kwao na familia zao kwa miaka nane nani anastahili kuwalipa fidia? Hawa wanastahili fidia,” alisema Mbowe.

Wakati huo huo, Mbowe aliiomba Serikali iwachukulie hatua, watu waliohusika kuwaweka mahabusu Masheikh hao, kinyume cha sheria.

“Masheikh wetu waliowekwa gerezani zaidi ya miaka nane, leo mmewaachia tunawashukuru kwa kufanya hivyo. Lakini basi nendeni hatua moja ya ziada, aliyewaweka ni nani, kwa sababu gani na hawa waliosababisha maumivu yao wanachukuliwa hatua gani?” alisema Mbowe na kuongeza:

“Hatuwezi tukaruhusu unaweka mtu miaka nane ndani, unakuja unamuachia unasema sina tena mashtaka ya kuendelea.”

DPP Mwakitalu aliwafutia viongozi hao 18 mashtaka, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kuwafutia mashtaka 14 kati ya 25 yaliyokuwa yanawakabili, tarehe 23 Aprili 2021.

Mahakama hiyo ilifuta mashtaka hayo, kwa maelezo kwamba hayakufanyika Tanzania Bara, hivyo haina mamlaka ya kusikiliza makosa yaliyofanywa visiwani Zanzibar.

DPP Mwakitalu amesema, mashtaka 11 yaliyosalia hayakuwa na nguvu, sababu iliyopelekea ofisi yake kuyafuta.

Masheikh hao wameachwa huru baada ya kusota mahabusu kwa miaka minane, tangu walipokamatwa katika nyakati tofauti kati ya 2012 na 2014.

Katika kesi hiyo, walikuwa wanadaiwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014, walijihusisha na makosa ya ugaidi, kinyume na kifungu cha 27 (c), cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

2 Comments

  • Tafadhali rejea kusoma alichosema DPP. Kesi hazijafutwa, bali zinabadilishwa kwa kuwa wengine wana mashtaka Zanzibar tu, wengine Bara tu, na wengine kote kuwili.
    Hizi siyo kesi za madai, zitachukuwa muda mrefu wasipotoa ushirikiano.
    Tuombe wayamalize!

  • Asante ndugu mbowe bongo sheria oi hakuna nahao sio wakwanza kukaa gerezani kwa mda mrefu hao ndani ya gereza wamewakuta watu hawaja uhukumia na wamewacha bado hawajauhukumiwa kwa maana io ndugu mbowe maombi ya sichague

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!