Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Lema na Jacob wakamatwa
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, Lema na Jacob wakamatwa

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salamaa nchini Tanzania, inawashikilia viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wakituhumiwa kuhamasisha maandamano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wengine ni; Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam, Boniface Jacob.

Chadema na ACT-Wazalendo wametangaza maandamano wametangaza kufanya maandamano ya amani yasiyo na kikomo wakipinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020.

SACP Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam

Vyama hivyo, vimepinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa madai uchaguzi uliosimamia uligubikwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni.

Katika matokeo hayo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya vyema kwa kujikusanyia viti vingi vya udiwani, ubunge na kuendelea kushinda nafasi ya urais ambapo mgombea wake, Dk. John Pombe Magufuli aliibuka na ushindi wa asilimia 84 ya kura 15 milioni zilizopigwa akimshinda Tundu Lissu aliyepata asilimia 13 ya kura zote.

Godbless Lema, Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema)

Kwa upande wa, Dk. Hussein Ali Mwinyi, alitangazwa na NEC kushinda ambapo leo Jumatatu ataapishwa kumrithi Rais Ali Mohamed Shein.

Leo Jumatatu tarehe 2 Novemba 2020, Kamanda Mambosasa amesema, mpaka sasa wanawashikilia watu saba wakiwemo viongozi hao watatu wa Chadema kwa mahojiano na baada ya hapo hatua zingine za kisheria zitafanyika.

“Kuna watu wamenyimwa kura kutoka majimbo yao na wamejikusanya katika kanda yetu. Godbless Lema amenyimwa kura Arusha amekuja Dar es salaam, Freeman Mbowe amenyimwa kura Hai wamekuja Dar es Salaam.”

“Mpaka sasa tunaendelea kufuatilia mmoja baada ya mwingine, Mbowe, Leman na Jacob tunawashikilia tangu jana usiku,” amesema Kamanda Mambosasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!