May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe kuzindua operesheni mpya, kufanyika nchi nzima

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

 

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, tarehe 27 Mei 2021 siku ya Alhamisi, anatarajiwa kuzindua ‘Operesheni Haki,‘ ambayo itafanyika nchi nzima. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne tarehe 25 Mei 2021 na Chadema, kupitia ukurasa wake wa Twitter, kampeni hiyo itazinduliwa jijini Arusha.

Taarifa ya Chadema imesema kuwa, lengo la operesheni hiyo ni kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, pamoja na uimarishwaji misingi ya haki nchini.

Sambamba na hilo, taarifa ya Chadema imesema, Mbowe ameendesha kikao cha Kamati Tendaji ya chama hicho, katika Kanda ya Kaskazini, kilichofanyika leo jijini Arusha.

“Leo Mei 25, 2021, Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe, ameendesha Kikao cha Kamati Tendaji ya Kanda ya Kaskazini, jijini Arusha,” imesema taarifa ya Chadema.

error: Content is protected !!