Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Mbowe kupata pigo lingine, mali zake sasa kupigwa mnada
Habari Mchanganyiko

Mbowe kupata pigo lingine, mali zake sasa kupigwa mnada

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

MALI za kampuni ya Mbowe Limited, inayomilikiwa na mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, zimapangwa kupigwa mnada, Jumamosi wiki hii. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na kampuni ya udalali ya Fosters Auctionare ya jijini Dar es Salaam, kufanyika kwa mnada huo, kunatokana na Mbowe kushindwa kulipa deni la Sh. 1.1 bilioni, anazodaiwa na Shirika la Nyumba la taifa (NHC).

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ya udalali, Joshua Mwaituka, amemueleza mwandishi wa MwanaHALISI ONLINE, mnada huo utafanyika kwenye ghala la NHC lililopo karibu na geti Na. 3, eneo la bandarini jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4 asubuhi.

Mwakituka ametaja baadhi mali zitakazopigwa manada, kuwa ni pamoja na taa, makabati, meza, makochi, viti na vitu vingine, majukwaa na vifaa vingine vilivyokuwa vikitumika kwenye ukumbi huo.

“Tumeelekezwa na NHC, kupiga mnada mali za kampuni ya Mbowe Limited, kufuatia wamiliki wake, kushindwa kulipa kodi kwa miaka 20. Thamani ya deni wanalodaiwa, ni Sh. 1.1 bilioni,” ameeleza Mwakituka.

Alipoulizwa kama wanadhani vitu wanavyouza, vitaweza kutosha deni wanalodai au wanafanya hivyo kwa misingi ya kisiasa, Mwakituka amesema, “tunauza kwa maelekezo ya mteja wetu NHC. Kama fedha itatosha au haitatosha, hilo tutalijua baadaye.”

Mbali na vitu ambavyo vilikuwa vinatumika kwenye ukumbi wa disco wa Bilicanas, vitu vingine vitakavyopigwa mnada, ni komputa, meza, makabati na viti, ambavyo vilikuwa vinatumiwa na kampuni ya Free Media, iliyokuwa inamiliki gazeti la Tanzania Daima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!