Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe kujiuzulu siasa 2020 Magufuli akishinda
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe kujiuzulu siasa 2020 Magufuli akishinda

Dk. John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) (Picha kubwa) na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe
Spread the love

FREEMAN Aikaeli Mbowe, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho amesema atajiuzulu kufanya siasa iwapo Rais John Magufuli atashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, anaandika Charles William.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ametoa kauli hiyo mbele ya wanachama wa Chadema wilayani Muheza Tanga ambapo yupo katika ziara ya kukagua uhai wa chama.

“Huyu atakuwa rais wa kwanza kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano tu. Na kama Magufuli akishinda tena uchaguzi mwaka 2020 mimi nitajiuzulu siasa,” amesema Mbowe.

Amesisitiza kuwa chama chake tayari kimeanza kujiandaa na uchaguzi wa 2020 kwani kumalizika kwa uchaguzi mmoja ni maandalizi ya uchaguzi mwingine.

Mbowe yupo ziarani mkoani Tanga, akifungua matawi ya chama hicho na kukagua uhai wa chama. Ameambatana pia na Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha).

Mbowe ndiye mwanasiasa pekee ambaye bado anafanya siasa miongoni mwa waasisi wa mwanzo kabisa wa Chadema.

Wengi wamekufa na wengine ni wazee kiasi cha kutoweza kumudu mikikimikiki ya siasa za majukwaani.

Hii ni ahadi ya pili ya Mbowe kujiuzulu siasa. Mara ya kwanza, mwaka 2014 aliahidi kujiuzulu siasa mwaka 2015 iwapo chama chake kingepata idadi ndogo ya kura za Urais na wabunge kuliko kilichopata mwaka 2010.

Hata hivyo Chadema kiliongeza Wabunge kutoka 49 mpaka 71 huku kura za urais zikipanda kutoka asilimia 26 kwa mwaka 2010 mpaka asilimia 40 kwa mwaka 2015.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!