October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe Kortini: Katika hili, namshangaa Rais Magufuli

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwamba anamshangaa Rais John Magufuli. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kiongozi huyo wa Chadema amesema, hamchukii Rais Magufuli ila anastaajabu namna anavyoshindwa kusimamia demokrasia.

Leo tarehe 8 Novemba 2019, akiongozwa na wakili wake Peter Kibatala, Mbowe alikuwa akiendelea kutoa ushahidi wake ambapo alinza kufanya hivyo tarehe 4 Novemba 2019.

Alitamka kauli hiyo baada ya Kibatala kumtaka Mbowe aeleze, kama anamchukia ama kumpenda Rais Magufuli.

Kwenye kesi hiyo namba 112/2018, Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kufanya mkusanyiko uliosababisha ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.

Washtakiwa wengine ni Dk.Vicent Mashinji, Katibu Mkuu-Taifa; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu – Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Pia wamo Ester Matiko Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Pia Mbowe amedai, mashtaka yanayowakabili na viongozi wenzake ni ya kisiasa zaidi, na kwamba yanawahifadhi waliokosa na kuwahukumu waliotendewa makosa.

Kiongozi huyo wa upinzani, ameiomba Mahakama ya Kisutu kupokea nyaraka mbalimbali kama kielelezo kwenye kesi hiyo.

error: Content is protected !!