July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe: Kikwete amalize aondoke

Viongozi wa Chadema Kanda ya Pwani wakiwa katika mafunzo kwa ajili ya kujiandaa na Uchaguzi Mkuu 2015, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba

Viongozi wa Chadema Kanda ya Pwani wakiwa katika mafunzo kwa ajili ya kujiandaa na Uchaguzi Mkuu 2015, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba

Spread the love

FREEMAN Mbowe-Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, amemtaka Rais Jakaya Kiwete amelize kipindi chake cha uongozi aondoke Ikulu badala ya kutumia ujanja wa kuchelewesha daftari la wapiga kura kujiongezea muda. Anaandika Pendo Omary…(endelea)

Mbowe anasema “Tunaitaka serikali iharakishe kuandikisha wapiga kura. Mpaka leo hatujamaliza Mkoa wa Njombe ambao hauna hata wapiga kura wengi kama Jimbo la Ubungo. Kwa miaka mitatu mfululizo tumembana Waziri Mkuu kuhusu Daftari bila mafanikio.”

Mbowe ametoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa Sabasaba PTA jijini Dares Salaam wakati akizindua mafunzo ya viongozi wa chama na timu za ushindi kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015.

Mpango huu unaanzia kanda ya Pwani ambapo viongozi wote wa chama na serikali za mitaa wamejumuika kupokea mafunzo haya na baadaye yataendelea kwenye kanda nyingine 9 za kichama.

Amesema “kampeni za uchaguzi huo, zitaanza tarehe 18 Agosti kwa mujibu wa Sheria. Hatupo tayari tarehe ya uchaguzi kuahirishwa 25 Oktoba, mwaka huu. Oktoba Kikwete nenda Msoga utuachie nchi yetu.”

Kauli ya Mbowe inakuja wakati ambapo, shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura kwenye daftari la kudumu kwa mfumo mpya wa Biometric Voters Registration (BVR) ikisuasua.

Aidha, taarifa za kuaminika ambazo zipo mpaka sasa na kuthibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ni kwamba mbali na kusuasua kwa shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura, NECT haikulifanyia marekebisho datari la awali kwa sababu halifai hata kwa marekebisho.

Hali hiyo imezua maswali wakadhaa kuhusu “Iwapo uchaguzi mkuu utafanyika mwaka huu au la!”.

Mbowe amesema mpango huo wa mafunzo ni kuwaandaa na kuwatayarisha viongozi wao. Kwamba “viongozi wanatayarishwa, hawazuki. Tunakwenda kutoa mafunzo kwenye kanda 10, majimbo ya chama 242 na ngazi za kata 4852, matawi 22,749 na misingi 64,803.”

Ametamba kuwa “tunakwenda kuwaandaa viongozi wetu tuwaache CCM wagombanie urais, sisi tutaleta wagombea makini.”

error: Content is protected !!