Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Dk. Mashinji wampigia saluti Zitto  
Habari za Siasa

Mbowe, Dk. Mashinji wampigia saluti Zitto  

Spread the love

HATUA ya Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo kushawishi na hatimaye waliokuwa viongozi waandamizi wa CUF kujiunga na chama chake, imepongezwa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Akimkaribisha Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) na timu yake aliyokwenda nayo Makao Makuu ya ACT-Wazalendo tarehe 18 Machi 2019, Zitto alisema hatua ya viongozi hao kujiunga na chama chake imepongezwa na vyama mbalimbali vya upinzani vikiongozwa na Chadema.

“Tunawashukuru Chadema kwa kutupongeza kwa hatua hii ya viongozi waandamizi wa CUF kuhamia ACT-Wazalendo. Nimefarijika kupata ujumbe wa pongezi kutoka kwa Mbowe (Freeman Mbowe-Mwenyekiti Chadema-Taifa), Dk. Mashinji (Dk. Vincent Mashinji-Katibu Mkuu Chadema), Mwalimu (Salum Mwalimu-Naibu Katibu Mkuu Zanzibar) na wengine.

“Niseme tu changamoto na mitihani ambayo vyama vya siasa hususani upinzani vinayopitia kwa sasa ndiyo inayotulazimisha tushirikiane kwa pamoja. Malaki ya wanachama wa CUF wanaohamia ACT-Wazalengo wana matumaini makubwa, tunapaswa kuyatekeleza,” alisema Zitto.

Zitto alisema, hatua ya Maalim Seif na timu yake kuhamia ACT-Wazalendo ni ya kuimarisha demokrasia Tanzania Bara na visiwani. “Na uimarishaji huu tutaufanya Bara na Visiwani.”

Akizungumza na wajumbe pia wanachama wa ACT-Wazalendo waliojumuika pamoja katika mapokezi ya Maalim Seif na timu yake, Zitto alisema lipo la kujifunza baada ya kiongozi huyo wa zamani wa CUF kujiunga na chama chake.

“Imetupa fundisho kwamba, ukiwa kiongozi uliye kwenye mioyo ya wananchi, hawawezi kukutupa. Tujenge uaminifu kwa wananchi wanaotupa dhamana,” amesema Zitto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!