Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe awazungumzia kina Lowassa, Sumaye
Habari za Siasa

Mbowe awazungumzia kina Lowassa, Sumaye

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, ametaka wafuasi wa chama hicho waliokimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM), wasidharauliwe. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe ametoa wito huo leo Alhamisi, tarehe 3 Juni 2021, jijini Mwanza, akizungumza na wanachama wa Chadema Kanda ya Victoria.

Miongoni mwa wanachama wa Chadema waliorejea CCM, ni aliyekuwa Mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Edward Lowassa. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye na aliyekuwa Mwenyekiti Chadema Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu.

Mwenyekiti huyo wa Chadema amesema, wanachama hao waliamua kwenda CCM, kwa kuwa mapigo ya upinzani yaliwashinda.

“Tusiwadharau wote waliotukimbia katikati ya vita hii, wengine mapigo yaliwashinda na ninyi ndugu zangu wa Mwanza lazima mtambue ya kwamba, mashujaa wanatambulika pale panapokuwa na matatizo makubwa, wao wanasimama ndiyo wanakuwa mashujaa,” amesema Mbowe.

Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu

Mbowe amesema, uongozi wa Tanzania wa Awamu ya Tano, chini ya Hayati Rais John Magufuli, ulikisaidia Chadema kuchuja wanachama waliokuwa na tamaa ya vyeo.

“Wale watu dhaifu dhaifu wote,wenye tamaa tamaa ya pesa na vyeo na wale watu waliokuwa upinzani kwa sababu ya kusaka vyeo, Magufuli alitusaidia chekecheke la kuwachekecha. Ambaye ameweza kubaki upinzani kwa miaka sita ya Magufuli, huyu ni shujaa,” amesema Mbowe.

Mwenyekiti huyo wa Chadema amesema, vyama vya upinzani ikiwemo chama chake, vilipitia misukosuko katika awamu hiyo, hivyo waliobaki upinzani baada ya awamu hiyo kupita ni mashujaa.

“Mashujaa ni Chadema jamani, watu waliokimbia upinzani ni njaa zao, wasingeweza kuzuia ule mziki wa mwendazake, haikuwa mchezo. Magereza tumekwenda lakini tumetoka mashujaa,” amesema Mbowe.

Frederick Sumaye, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani

Chadema ni miongoni mwa vyama vya siasa vya upinzani, vilivyoathirika na zoezi la hama hama ya wanachama, lililoibua kuanzia mwaka 2017, kwa maelezo ya kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli, aliyefariki akiwa madarakani tarehe 17 Machi 2021.

Magufuli aliyeongoza Tanzania miaka mitano na miezi mitano mfululizo (Novemba 2015-Machi 2021), alifariki dunia kwa ugonjwa wa moyo, kwenye Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam na mwili wake kuzikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita, tarehe 26 Machi mwaka huu.

Katika hamahama hiyo, Chadema ilipoteza wabunge kadhaa, ikiwemo aliyekuwa Mbunge wa Momba, David Silinde. James Millya (Simanjiro), Dk. Godwin Mollel (Siha), Joseph Mkundi (Ukerewe), Pauline Gekul (Babati Mjini) na Ryoba Marwa (Serengeti).

Wengine ni, Mwita Waitara (Ukonga), Peter Lijualikali (Kilombero).

Baada ya wabunge hao kujiuzulu na kuhamia CCM, chama hicho kiliwapitisha tena kugombea katika chaguzi ndogo, ambapo walifanikiwa kutwaa majimbo yao.

2 Comments

  • Asante ndugu mbowe kwa yote yanayo kukuta kwa kulinda usalama wa chadema kuchafuka kwa bahari sio mwisho wa safari lakini angalia hao uliona wa sije wakajitosa

  • Mbowe utajiponza sana kwa kutokuwa na sera nzuri utaded na presha huwezi kutuamisha kwa sera zako mbovu,
    Wewe ishauri serikali penye uzembe na ambapo imelegea kutoa hutoa huduma katika wananchi, hapo piga tuta kuelewa sana na hapo usimgusie kabisa hayati JPM utapata laana kubwa lakini ukiendelea kutoa porojo zako uchaguzi ujao hutapata hata jimbo moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!