May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe awachongea maafisa Takukuru kwa Rais Samia

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, awachukulie hatua maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), wanaotuhumiwa kuwabambikia watu kesi. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).

Mbowe ametoa wito huo leo tarehe 27 Mei 2021, akizindua Operesheni ya Haki, jijini Arusha, ambayo inatarajiwa kufanyika hivi karibuni katika kanda 10 za Chadema.

Mwanasiasa huyo ametoa wito huo, akizungumzia kauli ya Rais Samia, juu ya kesi 147 za kubambikizwa, zilizofutwa na Takukuru, hivi karibuni.

“Rais wa nchi anakiri hadharani kwamba, kwa miaka sita Takukuru wamesema wana kesi 147, za kuwasingizia Watanzania wamezifuta,” amesema Mbowe.

Rais Samia Suluhu Hassan

Mbowe amesema “Watanzania wameteswa, wako ndani, wamebambikiziwa kesi. Sawa mama kafanya jambo jema, lakini hao waliohusika kuwabambikia kesi wako ofisini. Hao wanastahili kuwepo katika magereza.”

Akizindua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Kurasini, mkoani Dar es Salaam, tarehe 18 Mei 2021, Rais Samia alisema Takukuru ilizifuta kesi hizo, baada ya kuiagiza izipitie upya kesi zake.

Ili ifute zilizokuwa za kubambikiza, kwa ajili ya kuondoa changamoto ya mrundikano wa mahabusu nchini.

Katika hatua nyingine, Mbowe amesema amemuandikia barua Rais Samia, akimuomba wafanye mazungumzo juu ya masuala mbalimbali, ikiwemo dosari zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, zilizosababisha athari nyingi ikiwemo uwepo wa wafungwa wa kisiasa.

“Nilimuandikia nikamwambia tuonane, tuzungumze, akasema tutazungumza. Akanijibu barua akisema mwenyekiti tutakuna na Chadema , tunasubiri wakati ukifika tuzungumze naye,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Kuna mambo mabaya yalifanyika nchini, tunataka tumwambie mambo yote ya uchaguzi yaliyofanyika. Vijana wetu zaidi ya 200 wako mabahusu na magereza hawana hatia.”

error: Content is protected !!