Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe atumia Sherehe za Uhuru kupenyeza ujumbe kwa JPM
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe atumia Sherehe za Uhuru kupenyeza ujumbe kwa JPM

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Maendeleo (Chadema) amesema sababu za kushiriki katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru ni kutoa ujumbe wa kuwepo kwa ulazima wa maridhiano, upendo na mshikamano. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mbowe alitoa ujumbe huo leo katika sherehe hizo baada ya kupewa nafasi na Rais John Magufuli kutoa salamu zake kama kiongozi wa chama cha Siasa, akiongozana na wanasiasa wengine waliohudhuria sherehe hizo.

Kiongozi huo wa Chadema alisema ameshiriki sherehe hizo ikiwa ni kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano upendo na mshikamano kwa Taifa letu, tuvumiliane, tukosoane na turuhusu demokrasia.

“Nimeshiriki, kama uthibitisho wa ulazima kuwepo maridhiano upendo na mshikamano kwa Taifa letu, tuvumiliane, tukosoane na turuhusu demokrasia, Rais una nafasi ya kipekee kujenga maridhiano katika Taifa, maana wengine wanalia, wengine wanafurahi.”

Mbowe ambaye ameshiriki katika maadhimisho hayo huku akiwa na kesi ya uchochezi mahakamani kwa zaidi ya miaka sasa, sambamba viongozi wenzake nane, lakini pia kukiwa na zuio la kutofanya mikatano ya hadhara.

Pia kumekuwa na malalamiko kwa vyama vya upinzani ya kubinywa kwa demokrasia nchini, hivyo ujumbe wa Mbowe unamuomba Rais Magufuli kujenga maridhiano kati ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na wapinzani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!