July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe atoa msimamo makongamano ya Katiba

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

 

FREEMAN Mbowe amesema, watafanya kongamano la Katiba jijini Mwanza keshokutwa Jumatano, tarehe 21 Julai 2021 na mikoa mingine yataendelea “hadi Katiba mpya itakapopatikana.”. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya kutofanyika kwa kongamano hilo juzi Jumamosi na kujikuta baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho zaidi ya 38 wakitiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.

Kati ya waliokamatwa ni Askofu wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Emmaus Mwamakula na Mhadhiri Mwandamizi wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azaveli Lwaitama ambao wasisota rumande hadi jana jioni Jumapili, walipoachiwa.

Mara baada ya kutofanyika kwa kongamano hilo kwa madai ambayo polisi wamesema hawakuwa na taarifa, Mbowe aliyekuwa katika maombolezo ya msiba wa kaka yake, Charles, mkoani Kilimanjaro, alisitisha na kwenda Mwanza.

DK. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri mstaafu

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Jumatatu, tarehe 19 Julai 2021, makongamano ya Katiba yataendelea kufanyika nchi nzima hadi siku itakayopatika katiba mpya.

“Hatutaondoka hapa Mwanza na wiki hii tufanya kongamano kubwa hapa Mwanza, sisi viongozi hatutaondoka Mwanza na kama polisi wanataka kutukamata basi waanze kunikamata mimi Mbowe,” amesema Mbowe

Katika kusisitiza hilo amesema “tutafanya makongamano haya nchi nzima hadi tupate katiba mpya kwani Katiba ya nchi ni katiba ya Taifa, haipaswi kuwa Katiba ya chama na haipaswi kuwa na kiongozi yoyote atakayezuia mjadala wa Katiba.”

Mbowe amesema, harakati za kudai katiba mpya si ya chama cha siasa peke yake “na ili polisi wasituondoe kwenye mstari, kwa sasa mwanachama wetu akiwekwa ndani, hatutamwekea dhamana. Kwani mikutano hii tunaifanya kwa mujibu wa Katiba na sheria.”

error: Content is protected !!