March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe atinga mahakamani kwa Sugu

Freeman Mbowe akiwasili mahakamani kusikiliza kesi ya Sugu

Spread the love

MWENYEKITI WA CHADEMA, Freeman Mbowe amewasili katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, kuhudhuria kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katiku Mkuu wa Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, inayoendelea mahakamani hapo. Anaripoti Mwandishi Wetu.

Sugu na Masonga wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambayo waliyatoa katika mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana wakiwa viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Mbowe alihudhuria mahakamani leo Jumatano Januari 24, 2018 kwa ajili ya kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge huyo na mwenzake kwa lengo la kuwatia nguvu na kuhakikisha haki inatendeka kwa watuhumiwa hao.

Mwenyekiti Mbowe ambaye ameongozana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagenda ameingia majira ya saa 3.30 asubuhi hii katika viunga vya mahakama kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo na tayari ameingia kwenye chumba cha mahakama.

Sugu pamoja na Masonga walifikishwa mahakamani hapo kwa mara kwanza Januari 19, 2018 lakini  mahakama ilizuia dhamana zao na kuwarejesha rumande hadi.

Siku hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite alitoa uamuzi wa kuwarejesha rumande, kwamba kesi hiyo inatakiwa isikilizwe mfululizo kwa muda mfupi na washtakiwa wakiwa wanafika mahakamani hapo wakitokea mahabusu.

error: Content is protected !!