Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe ‘apinduliwa’ bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe ‘apinduliwa’ bungeni

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

WABUNGE 12 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), waliorejea bungeni kabla ya muda waliokubaliana na wenzao kumalizika, wameunda uongozi wao bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya Katibu wa Bunge mjini Dodoma zinasema, kambi hiyo mpya ya upinzani, inaongozwa na Mbunge wa Bukoba Mjini, Willifred Muganyizi Lwakatare.

Akizungumza na MwanaHALISI mmoja wa wabunge waliorejea bungeni amesema, wameamua kuchukua hatua hiyo, ili kurahisisha kazi zao na kuwa na mawasiliano ya uhakika na ofisi ya Spika.

“Ni kweli, sisi tuliyobaki bungeni, tumeamua kuunda uongozi wetu. Tumemchagua Lwakatare kuwa kiongozi wetu (KUB). Na kesho tunakwenda kwa Spika Ndugai, ili kumtaarifu,” ameeleza.

Lwakatare ni mmoja wa wabunge wa Chadema walioamua kurejea bungeni, kupinga maagizo ya mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.

Wilfred Lwakatare, Mbunge wa Bukoba Mjini

Kambi ya Lwakatare imeundwa kuchukua nafasi ya ile iliyokuwa inaongozwa na Freeman Mbowe, ambaye kwa sasa yuko nje ya Bunge akijitenga na maambukizi ya Corona.

Wengine waliochaguliwa kuunda uongozi wa kambi hiyo, ni Latifa Chande ambaye anakuwa katibu na Anthony Komu, aliyefanywa kuwa Mnadhimu wa kambi hiyo.

Viongozi hao watatu ndio watakaongoza kambi ya upinzani bungeni hadi hapo Freeman na wenzake watakaporuhusiwa kurejea bungeni.

Hata hivyo Lwakatale, alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo, amekana madai hayo na kueleza kuwa walichounda wao, ni uongozi wa muda wa kuwasaidia kufanikisha shughuli zao.

Alisema, “tulichounda jana, ni uongozi wa muda ambako tumeteuwa Mmadhimu wa Kambi ya Upinzani ambaye atakuwa na kazi ya kutusaidia kutuunganisha pamoja.”

Aliongeza: “Hatujampindua mwenyekiti na hatuko hapa kumpindua yeyote. Tuko bungeni kuwakilisha wananchi na ili tufanye kazi hiyo, sharti tuwe na uongozi. Hilo ndilo tulilolifanya.”

Spika wa Bunge, Job Ndugai alitangaza jana Jumanne kuwa wabunge wa Chadema wasiporejea bungeni hadi kumalizika siku 14 walizojipa, hawataruhusiwa kuingia bungeni, hadi hapo watakapopima afya zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!