July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe apeleka “moto” Kanda ya Ziwa

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara

Spread the love

KATIKA kujiimarisha kukamata dola Oktoba mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameanza ziara ya siku sita mikoani, ukiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa program ya mafunzo kwa viongozi wa chama…Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Programu hiyo maarufu kama ‘Fast Truck Program- (FTP)’, ilizinduliwa kwa ajili ya mafunzo ya uzalendo kwa vijana wa chama ikiwa ni mwendelezo washughuli ambayo imekuwa ikifanywa tangu Januari mwaka huu.

Wakati Mbowe akielekea mikoani kwa kazi hiyo, viongozi waandamizi wa kitaifa nao wametawanyika katika kanda mbalimbali za kichama, wakiendelea kutoa mafunzo kwa viongozi wao wa serikali za mitaa, ambayo yalizinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

Afisa habari wa Chadema, Tumain Makene, ameliambia MwanaHALISIOnline kuwa, leo Mbowe ameanza ziara yake wilayani Nzega-Tabora ambapo atazindua FTP eneo la Ndala kisha atahutubia mkutano wa hadhara.

Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) linaloundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, kesho atakuwa Itirima-Bariadi na kesho kutwa atakuwa Ukerewe mkoani Mwanza.

Makene amesema “siku inayofuata atakuwa Bukoba Mjini kisha wilayani Kyerwa huko huko mkoani Kagera. Kote huko atafanya uzinduzi wa FTP asubuhi na jioni atahutubia mikutano ya hadhara”.

Ameongeza kuwa, katika maeneo yote, Jeshi la Polisilimealikwa kutoa elimu ya ulinzi shirikishi na polisi jamii. Pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nayo imealikwa kutoa elimu ya kupambana na rushwa hasa wakati huu wa uchaguzi.

Kuhusu programu ya uzinduzi wa mafunzo ya kukiandaa chama kwenda kushika dola na kuongoza serikali, Makene amesema “Makamu Mwenyekiti wetu, Prof. Abdallah Safari, atakuwa Korogwe Mjini ambapo atazindua mafunzo hayo kwa viongozi wa Korogwe mjini na vijiji kisha atahutubia mkutano wa hadhara.”

Makene amefafanua kuwa, Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika amezindua mafunzo Bariadi kisha akaelekea Maswa.

“Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu, amezindua mafunzo mjini Mbalizi mkoani Mbeya kisha akahutubia mkutano wa hadhara mjini Njombe,” amesema Makene.

error: Content is protected !!