Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbowe apate pigo jingine, baba yake mdogo afariki dunia
Habari Mchanganyiko

Mbowe apate pigo jingine, baba yake mdogo afariki dunia

Spread the love

 

MANASE Alphayo Mbowe, baba mdogo wa Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe, amefariki dunia asubuhi ya leo Ijumaa, tarehe 23 katika Hospitali ya Machame mkoani Kilimanjaro, alikokuwa anapatiwa matibabu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endele).

Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo Ijumaa na James, mtoto wa Freeman wakati akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu akisema, alishtushwa baada ya kusikia tuhuma zinazomkabili mwanae za ugaidi

James amesema, babu yake huyo alifariki dunia akipatiwa msaada wa kupumua kwa kutumia mashine ya oksijeni, hospitalini hapo lakini “leo asubuhi akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo amefariki dunia.”

James amesema, taratibu za mazishi yake zitatangazwa baadae baada ya familia kukutana.

Amesema, enzi za uhai wake, babu yake huyo aliwahi kufanya kazi serikalini ikiwemo ofisi ya Rais. Ameacha watoto watano, wa kike mmoja na wa kiume wanne.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Kifo hicho ni pigo jingine kwa Mbowe ambaye tangu usiku wa kuamkia juzi Jumatano tarehe 21 Julai 2021, amekuwa mikononi mwa jeshi la polisi.

Mbowe na wenzake 11, walikamatwa wakiwa katika Hotel ya Kingdom jijini Mwanza, walipokwenda kwa ajili ya kufanya kongamano la kudai katiba mpya.

Hata hivyo, kongamano hilo halikufanyika kutokana na kutiwa mbaroni. Wakati wenzake 11 wakibaki Mwanza, Mbowe alisafirishwa hadi Dar es Salaam ambapo polisi walikwenda kufanya upekunzi nyumbani kwake, Mikocheni.

Na jana Alhamisi, Jeshi la Polisi Tanzania lilisema linamshikiliwa mbowe kwa tuhuma za kupanga njama za mauaji ya viongozi wa serikali na ugaidi.

Huu ni msiba wa pili kumkuta Mbowe ndani ya wiki chache, baada ya kaka yake, Charles Mbowe, kufariki dunia, tarehe 8 Julai 2021, na mwili wake kuzikwa nyumbani kwao Machame mkoani Kilimanjaro, tarehe 12 Julai 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!