July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe apata ulinzi wa Polisi

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

JESHI la Polisi wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro, limevamia mkutano wa ndani wa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni, kumlinda kiongozi huyo na wafuasi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Tukio hilo limetokea leo tarehe 30 Septemba 2019 baada ya Lengai Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai kuagiza polisi kufika katika mkutano huo, kwa ajili ya kufuatilia agenda zake.

Ole Sabaya ameeleza kuwa, amechukua hatua hiyo kwa ajili ya kumlinda Mbowe, viongozi na wafuasi wa Chadema waliohudhuria katika mkutano huo, uliofanyika katika ofisi za Chadema za Wilaya ya Hai.

Mkuu huyo wa wilaya amesema, wanaoshiriki katika mkutano huo, hawana sababu ya kutaharuki kama wamefanya mkutano huo kwa nia njema.

error: Content is protected !!