Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe apata ugonjwa akiwa rumande
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe apata ugonjwa akiwa rumande

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mwenyekiti wake Taifa, Freeman Mbowe, anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kwa tuhuma za ugaidi, anaumwa. Anaripoti Mwandishi wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu, tarehe 26 Julai 2021 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema.

“Leo tumepokea taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia, ambao walimtembelea mwenyekiti katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay asubuhi hii, kuwa mwenyekiti anaumwa na tayari ameshalijulisha Jeshi la Polisi kuhusu kuumwa. Akiwataka wampeleke hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi na matibabu,” amesema Mrema.

MwanaHALISI Online imemtafuta kwa simu mtoto wa Mbowe, James Mbowe, ambaye amesema Polisi wamemtoa baba yake katika kituo hicho na kumpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo, James hakutaja hospitali rasmi ambayo Mbowe amepelekwa.

Kwa sasa wamemchukua, wamemtoa Polisi wanampeleka hospitalini. Lakini hawajasema hospitali gani. Yawezekana kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili au Agha Khan,” amesema James.

Alipoulizwa ugonjwa unaomsumbua Mbowe, James amesema kwa sasa haifahamiki, bali itajulikana pindi mwanasiasa huyo atakapofikishwa hospitalini.

“Nafikiri baada ya kufika hospitalini ni rahisi kufahamu kinachomsumbua, siku zote wamemshikilia hatujajua nini kimempata mzee,” amesema James.

MwanaHALISI Online imemtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Kinondoni, Ramadhan Kingai, kupata undani wa taarifa hizo, ambaye amejibu “ naomba unipigie baadae kidogo, nitakufahamisha.”

Mbowe yuko rumande tangu tarehe 21 Julai 2021, alipokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, kisha kusafirishwa kuelekea katika Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kwa ajili ya mahojiano dhidi ya tuhuma za ugaidi zinazomkabili.

1 Comment

  • ILE MBWE AZIDI KUWA KIONGOZI KINDAKINDAKI LAZIMA APITE NJIA ALIZOPITIA ALMARHUM MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AMA NELSON MANDELA.KIZA KINENE ALFAJIRI INAKARIBIA PEOPLE POWER USHINDI NI LAZIMA TUTASHINDA TUUUU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

error: Content is protected !!