Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe aomba radhi wanawake kwa kuwaita ‘mademu’
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe aomba radhi wanawake kwa kuwaita ‘mademu’

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amewaomba radhi wanawake kwa kuwaita mademu wakati anahutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Jumamosi iliyopita jijini Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani Mara leo tarehe 23 Oktoba 2023, Mbowe amesema kauli hiyo imewakwaza baadhi ya watu kwa sababu haikuwa ya staha.

“Kuna jambo napenda niliseme, nilizungumza katika mkutano siku mbili zilizopita nikazungumza katika kujenga hoja yangu nikajenga hoja nikawazungumzia mama zetu kama mademu, kuna watu nimewakwaza kidogo na mimi naelewa haikuwa lugha ya staha lakini kiongozi mstaarabu hawezi kuogopa kuomba radhi, wale wote waliofikiri lugha ile niliitumia vibaya naomba radhi ndugu zangu,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema chama chake kinawapenda na kuwathamini wananwake, hivyo kitaendelea kuimarisha usawa wa kijinsia.

Akizungumzia ajenda za kitaifa, Mbowe amesema nchi inahitaji katiba mpya iliyo bora ambayo itakuwa na uwezo wa kuwawajibisha viongozi wanaokiuka maadili yao ya kazi.

“Lazima tupate katiba mpya ambayo kiongozi akifanya maamuzi ya kihuni lazima yakamtafune mbele ya maisha, ili kila mmoja anayepewa ofisi ya umma ajue anakabidhiwa roho za watanzania, hayo ndiyo mabadiliko ya msingi tunayotaka katika nchi yetu,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Tunataka viongozi wetu hata wa Chadema wanapokamata madaraka ya umma wawe na hofu ya Mungu wanapoongoza, katiba iwadhibiti viongozi wetu wanaotumia madaraka vibaya kwa kutoa amri za watu kuuawawa na kujeruhiwa, watambue kwamba mbele ya safari watajibu maswali.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

error: Content is protected !!