February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe anena mazito wakili wao kujitoa

Spread the love

BAADA ya Jeremiah Mtobesya, wakili anayetetea viongozi waandamizi wa Chadema wanaokabiliwa na kesi ya jinai namba 112, kujitoa katika kesi hiyo. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa ameendelea kuonyesha kutoridhishwa kwake na uendeshaji wa Hakimu Wilbard Mashauri. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 23 Agosti, 2018, Mbowe amesema kitendo cha wakili huyo kujitoa katika kuwatetea kinadhihirisha kile alichokiita kuwa, Hakimu Mashauri anaendesha kesi yao kwa kufuata maagizo yaliyotoka juu badala ya kufuata sheria.

Mbowe ameeleza kuwa, malalamiko yao kuhusu kutokuwa na imani na Hakimu Mashauri hayamaanishi kama wanaogopa kufungwa, bali hawataki kufungwa kwa makosa wasiyokuwa na hatia nayo.

Mbowe amedai kuwa, Hakimu Mashauri anaiendesha kesi hiyo haraka haraka kana kwamba anapokea mashinikizo kutoka juu.

“Tuliwahi kufikia hatua ya kumkataa hakimu kutokana na mwenendo wake unaonyesha kama anaendesha kesi kwa mashinikizo. Hatua hii imechosha mawakili wetu. Wakili amejitoa bado hakimu akataka kesi kesho iendelee,” amesema.

Wakili Mtobesya alijitoa katika kesi hiyo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuyatupilia mbali maombi ya washtakiwa ya kutaka kesi hiyo iahirishwe. Ili kusubiri maombi yao ya rufaa yaliyopo katika mahakama ya rufani.

Viongozi hao wa Chadema wapatao tisa wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo ya kufanya mkusanyiko kinyume na sheria.

error: Content is protected !!