MWENYEKITI wa chama kikuu cha upinzani Tanzania- Chadema, Freeman Mbowe amemtumia salamu Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kufuatilia kifo cha Rais John Pombe Magufuli (61). Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).
Rais Magufuli, alifikwa na mauti saa 12 jioni ya Jumatano tarehe 17 Machi 2021, Hospitali ya Mzena, Makumbusho, mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo wake.
Mama Samia, ametangaza siku 14 za maombolezo na bendera zitapepea nusu mlingoti huku taratibu za mazishi zitatolewa baadaye.
Katika salamu hizo ambazo amezitoa Mbowe, ametoa pole kwa Mama Samia ambaye ataapishwa wakati wowote kuwa Rais, Janeth, Mjane wa Rais Magufuli, familia na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Pamoja na kuwa katika wakati wa majonzi na maombolezo ya kitaifa, kifo hiki kinatukumbusha na kutufundisha thamani ya maisha na utu wetu na kuwa na upendo katika kutenda yaliyo mema wakati wa uhai wetu hapa duniani,” amesema Mbowe
Amesema, kipindi hiki cha maombolezo, “tukitumie kufungua ukurasa mpya wa kulirejesha taifa kuwa moja na lenye kulinda na kuheshimu uhuru, haki, utawala wa sheria, demokrasia na maendeleo ya watu.”

Mbowe amesema,”ni imani yetu, kuwa Rais ajaye, Mama Samia atalinda misingi hiyo na ataliongoza Taifa kufikia maridhiano ya Kitaifa.”
“Tuna amini, Samia alikuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba, atalipatia Taifa katiba mpya iliyotokana na maoni ya wananchi.”
Ni utu kwa wakati huu kuutumia kimajonzi na sio kisiasa, wapinzani tuwe waungwana ktk Salam zetu, Uma unawatazama hekima zenu.
Asante ndugu mbowe lakini fikiria kwanza unachoongea kabla hujaongea tabia njema ndio siraha
Mbowe umewahi, kumbuka harakaharaka haina baraka