Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe amchongea Magufuli kwa wananchi
Habari za Siasa

Mbowe amchongea Magufuli kwa wananchi

Dk. John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) (Picha kubwa) na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe
Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amewataka watanzania kutokuogopa kumkosoa Rais John Magufuli pale anapokosea, anaandika Hellen Sisya.

Mbowe ameyasema hayo mapema leo hii katika hoteli ya Protea iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa endapo taifa litakuwa na watu waoga, basi kuna uwezekano wa taifa hilo kutawaliwa na dikteta.

“Anapostahili pongezi tumpe pongezi, anapostahili lawama tumpe lawama bila kuogopa. Tukiwa taifa la watu waoga Mwalimu Nyerere alituasa tutatawaliwa na dikteta “ amesema Mbowe.

Aidha, Mbowe amesisitiza kuwa watanzania wanapaswa kutambua kuwa kauli za Rais Magufuli sio sheria za nchi.

“Rais apongezwe pale anapofanya jambo jema. Lakini afanye jambo jema kwa misingi ya katiba, sheria pamoja na mikataba ambayo tunaingia. Tusiwe wepesi kumshangilia Rais kwa kila analolizungumza tukidhani ni jambo jema,” amesisitiza Mbowe

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!