December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe alivyowasalimia kortini, nao wamwombea

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema akiingia mahakamani

Spread the love

 

KESI ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, inaendelea leo Jumanne, tarehe 23 Novemba 2021. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mara baada ya Mbowe na wenzake Adam Kasekwa, Mohamed Ling’wenya na Halfan Bwire walipofika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyopo Mawasiliano jijini Dar es Salaam, asubuhi ya leo Jumanne, tarehe 23 Novemba 2021, wamepokelewa na baadhi ya wanachama wa Chadema waliokuwa nje.

Mbowe na wenzake baada ya kufika karibu na geti la kuingilia mahakamani, akiwa mwenye nyuso ya tabasamu Mbowe aliwasalimia “hamjambo” kisha nao wakaitikia “hatujambo shikamoo” na sauti ya mmoja wa wanawake waliokuwepo akasikika akisema “Mungu akulinde na Mungu awalinde wote” na mwingine akasema “amina”

Aidha, Mbowe na wenzake walipoingia ndani ya chumba cha mahakama, Mbowe aliwasalimia “Bwana Yesu asifiwe” wakaitikia “amina” akasalimia tena As-salamu alaykum wakaitkia
akasalimia tena tumsifu yesu na wakaitikia tena na kabla hajaa amasema “siku njema kwenu.”

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Joachim Tiganga inaendelea kwa shahidi wa tatu wa Jamhuri, askari polisi H4347 Goodluck (32) wa kituo kikuu cha Polisi Arusha, idara ya upelelezi wa makossa ya jinai yupo kizimbani akitoa ushahidi wake.

Anatoa ushahidi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi ya kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa, Mohamed Ling’wenya yasipokelewe mahakamani kama kielelezo cha mahakama wakidai hakuwahi kutoa maelezo bali alilazimishwa kuyasaini.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!