Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe ‘ajisalimisha’ kwa Rais Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe ‘ajisalimisha’ kwa Rais Magufuli

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemwandikia barua Rais John Pombe Magufuli, kikimtaka kuunda tume ya mardhiano, ili kuliondoa taifa katika kile ilichoita, “mkwamo wa kisiasa.” Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijiji Dar es Salaam, leo Jumatatu, tarehe 3 Februari 2020, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema, Rais Magufuli ana wajibu wa kurejesha umoja wa kitaifa, amani na mshikamano nchini.

Kwa mujibu wa Mbowe, taifa hili linapitia katika sintofahamu kubwa, ikiwamo  kuzorota kwa mahusiano kati ya vioongozi wa vyama vya siasa na jamii, pamoja na kuwapo kwa viashiria vya kutengwa na jumuiya ya kimataifa.

Amesema, tayari chama chake, kimemuandikia barua Rais Magufuli, baada ya kujiridhisha kuwa taifa la Tanzania, linapita katika sintofahamu kubwa pamoja na kukabiliwa na hatari ya kuvurugika umoja wa kitaifa.

Kuibuka kwa Mbowe kutaka Rais Magufuli kufanya mkutano na viongozi wa upinzani kwa lengo la kujadiliana, kumeshangaza baadhi ya wachambuzi wa kisiasa, kufuatia hatua ya kiongozi huyo, kupinga wito wa kukutana na Rais Magufuli.

Miongoni mwa watu waliomtaka Mbowe kukutana na Rais Magufuli, ni pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai; aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Bw. Edward Lowassa; baadhi ya wabunge wa Chadema na jamii za kimataifa.

Katika barua hiyo, Mbowe amesema, kabla ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa Oktoba mwaka huu, Chadema kimetaka kufanyika “mambo matatu muhimu kwa maslahi ya taifa.”

Ametaja mambo hayo kuwa ni marekebisho madogo ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ili kuruhusu kuwapo kwa Tume Huru ya Uchaguzi, pamoja na sheria yake ya uchaguzi ya mwaka 1984; na sheria nyingine mbalimbali, ili kuwezesha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, kuweza kuwa huru na haki.

Jingine lililotajwa kwenye barua hiyo, ni kurudiwa kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji wa Novemba 2019.

Pendekezo jingine, lililomo kwenye barua ya Mbowe kwenda kwa Rais Magufuli, “ni kuundwa kwa Tume ya Maridhiano ya Kitaifa.”

Amesema, “kuna mfarakano mpana unaendelea kulitafuna kwa taifa letu. Umoja wetu wa ndani, umeanza kumomonyoka. Hili kama taifa, halipaswi kuendelezwa.”

Akisoma barua hiyo iliyokwendwa kwa rais mbele ya waandishi wa habari, Mbowe alisema, “kufuatia changamoto hizo, serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka, hususan katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Amesema: “Chadema kama chama kikuu cha upinzani, inaamini kuna kila sababu za kuchukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto hizi. Nawe kama rais, una mamlaka yote ya kuanzisha mchakato wa kurudisha mtengamano wa nchi yetu.”

Ameongeza: “Huu ni mwaka wa uchaguzi, unahitaji busara uelewa na uvumilivu ili kuivusha nchi salama. Kwa hali ilivyo sasa, kuna kila aina ya viashiria vya uwepo wa machafuko ya kisiasa kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

“Kama hatutazika viburi vyetu vya kiitikadi na badala yake tukasimama kama taifa, kuruhusu haki na demokrasia ya kweli kutamalaki katika kipindi chote cha mwaka huu wa uchaguzi, basi taifa letu tunaweza kuliingiza kwenye shida.”

Barua ya Mbowe kwenda kwa Magufuli, imenakiriwa kwa Spika wa Bunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!