Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Tangulizi Mbowe aishiwa uvumilivu kortini
Tangulizi

Mbowe aishiwa uvumilivu kortini

Spread the love

IDADI kubwa ya mashahidi wa upande wa Jamhuri kwenye kesi ya uchochezi namba 112/2018, inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake, imeibua mjadala. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Mbowe ambaye ni mshtakiwa namba moja kwenye kesi hiyo pia Mwenyekiti wa Chadema Taifa, alilazimika kusimama na kuomba mabahakama iamuru upande wa Jamhuri kutaja idadi ya shahidi wake.

Ni baada ya upande wa Jamhuri ulioongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi kuiomba mahakama hiyo iahirishe usikilizwaji wa shauri hilo, kutokana na shahidi namba nane wa Jamhuri kupata udhuru kutokana na majukumu ya kazi.

Kwenye kesi hiyo, washtakiwa ni Mbowe mwenyewe; Vicent Mashinji, Katibu Mkuu; John Mnyika, Naibu Katibu-Bara; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu -Zanzibar na Halima Mdee, Mbunge wa Kawe.

Wengine ni Peter Msigwa, Mbunge wa  Iringa Mjini; John Heche, Mbunge Tarime vijijini; Ester Bulaya, Mbunge wa  Bunda Mjini na Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini.

Mbowe ametoa ombi hilo leo tarehe 10 Septemba 2019, ambapo Wakili Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ameieleza mahakama hiyo, kwamba shahidi huyo ambaye ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Bernard Nyambari, Mkuu wa Upelelezi Wilaya wa Kipolisi Mbagala wakati akipokea wito wa mahakama kuja kutoa ushahidi, alikuwa ana operesheni ya kipolisi.

Baada ya Wakili Nchimbi kutoa ombi hilo, Mbowe alisimama na kuiomba mahakama hiyo iamuru upande wa jamhuri kutaja idadi ya mashahidi wake.

Baada ya ombi hilo, Wakili Nchimbi aliieleza mahakama hiyo kuwa sheria haielezi kama kuna ulazima idadi kamili ya mashahidi kutajwa mahakamani, na kwamba wataendelea kuleta mashahidi kadri mahakama hiyo itakaporuhusu.

Kifuatia hoja hizo, Hakimu Simba alikubaliana na hoja ya Wakili Nchimbi akisema kwamba sheria inaruhusu kutotaja idadi ya mashahidi.

Awali, Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini ambaye ni miongoni mwa washtakiwa, alilalamikia hatua ya kesi hiyo kuahirishwa akidai kwamba hawatendewi haki.

Naye John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini amedai kwamba kitendo cha kesi hiyo kuahirishwa kinalenga kuwakomoa, huku akisema kwamba anatumia fedha nyingi kwa ajili ya kulipa gharama za malazi.

“…. kama binadamu, hapa sina makazi ni gharama kukaa hapa. Tunakuwa kama wafungwa nje ya muda, inakuwa kama tunakomoana,” amedai Heche.

Hakimu Simba amesema utaratibu wa mahakama hiyo unaelekeza kesi kumalizika kwa wakati, na kuusisitiza upande wa jamhuri kuleta mashahidi ili kesi hiyo iishe na kuondoa malalamiko.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi kesho tarehe 11 Septemba 2019 majira ya saa 4.30 asubuhi.

ASP Nyambari mbele ya Hakimu Simba aliongozwa na Wakili  wa Serikali Mkuu, Dk. Zainab Mango kutoa ushahidi wake, baada ya shahidi namba saba kumaliza kutoa ushahidi wake.

Hata hivyo leo upande wa Jamhuri umemaliza kuwasilisha ushahidi wa shahidi wa saba uliotolewa na Victoria Wahenge, Ofisa wa Uchaguzi katika Manispaa ya Kinondoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Rais Samia amng’oa Matinyi Maelezo, ateua viongozi mbalimbali

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwamo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia: Wakuu wa mikoa, wilaya wanaendeleza ubabe

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema bado wakuu wa wilaya na...

error: Content is protected !!