Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe aibua mazito risasi ya Akwilina
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe aibua mazito risasi ya Akwilina

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kuwa jeshi la Polisi limewajeruhi waandamanaji wa tano wa risasi za moto huku moja ikimpata Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT), Akwilina Akwilini zilizokuwa zikiwalenga wao. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbowe amewaambia waandishi wa Habari leo, kuwa Polisi walifyatua risasi za moto ambayo zilikuwa zinawalenga moja kwa moja waandamanaji na siyo juu kama ilivyodaiwa na Jeshi la Polisi.

Maandamano hayo yalifanyika Februari 16, mwaka huu ambapo Akwilini aliyekuwa akitoka Mabibo akielekea Makumbusho akiwa kwenye daladala alifariki kwa kupigwa na risasi ya moto inayotokana na maandamano hayo.

Mbowe aliyekuwepo kwenye maandamanano hayo amesema kuwa zilirushwa risasi zilizowalenga wao. “Sisemi kama zilikuwa zinanilenga mimi lakini zililengwa kwetu waandamanaji.”

Amesema kuwa risasi hizo ziliwapiga waandamanaji watano ambao hadi leo hawakupewa dhamana na hawakufikishwa mahakamani.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwashikilia majeruhi hao ili wasitoke nje wakaonekana kwenye vyombo vya habari.

‘’Unatumiaje siraha za moto kuzuia maandamano ya amani. Fanya hivyo halafu waache majeruhi wakajipatie matibabu lakini bado munawashiria,’’ amesema Mbowe.

Ameeleza kuwa chama hicho kupitia mawakili wake wamefungua shauri mahakamani la kuwashinikiza polisi kuwapeleka mahakamani wafusi hao.

Wakati huohuo, Mbowe amedai kuwa vyombo vya usalama vinaratibu mipango ya kuwabambikia kesi za ugaidi, mauaji na uhaini viongozi wa Chadema.

Amesema kuwa kuibuka Cyplian Musiba na madai yake ni kuandaliwa kwa tuhuma hizo na kwamba maneno hayo ya yalikuwa sio yake ni maneno ya kulishwa, lakini watatii sheria na kwamba wataitetea haki na demokrasia kwa misingi ya haki.

Mbowe ameeleza kuwa vurugu hizo zinasababishwa na watendaji wa juu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) kutokana na kushindwa kusimamia haki.

“Kailima (Ramadhani) Mkurugenzi wa Uchaguzi tumemuandikia barua, tumemfuata ofisini kwake tumempigia simu yake tumemueleza vitu ambavyo vilikuwa vikionesha uchaguzi utaharibika, hakutaka kuelewa kwa vile anapokea maagizo kutoka serikalini hakutusikiliza.

“Hakuna wakati wowote katika historia ya uchaguzi wa nchi hii ambapo tuna tume hopeless, Mkurugenzi hopeless, kama kipindi hiki, angalau zamani walikuwa wanaiba kiakili lakini wao wanaiba kitoto kijinga kipumbavu, kumfurahisha bwana mkubw, aliyesema hataki kuona mpinzani anatangazwa kuwa mshindi,” amesema Mbowe kwa uchungu.

Mbowe amesema kuwa kama Tume haitaki kutambua nafasi ya upinzani nchini haina haja ya kufanya uchaguzi kutokana na hasara zinazotokea, kuliwa kwa watu, kuumizwa watu.

Amesema kuwa waliwasiliana Mkurugenzi Kailima kumjuza kuwa wasimamizi wa uchaguzi kuwa ni makada Chama cha Mapinduzi (CCM) lakini hakuchukua hatua yoyote.

“Ndugu zangu chaguzi zote zitaendelea kuzaa majeraha maumivu kama hatua serious hazikuchukuliwa kwa sababu hawa wenzetu hawana aibu, wamejipanga wanalindwa na dola…. Walitunyima vitambulisho vya mawakala wetu ili waibe kura ndicho walichofanya,” amesema Mbowe.

Kwa upande mwingine Mbowe amesema kuwa hukumu ya Mbunge wa Mbeya Jesoph Mbilinyi na Katibu wa Chama hicho Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga imefanywa kwenye ushirika wa viongozi wa CCM, watendaji wa serikali pamoja idara ya Usalama wa Taifa kwa kumtumia hakimu.

Mbowe amesema kuwa licha chama hicho kuheshimu muhimili wa Mahakama kutokana upekee wake katika kutoa haki kwenye nchi lakini wapo mahakimu wanaotumika vibaya kupindisha sheria kwa visasi.

Amesema kuwa wao kama chama walishapata taarifa siku nne kabla siku ya hukumu kuwa mipango iliyopangwa ni kuwafunga viongozi hao.

“Polisi na vikosi vya usalama vilikusanywa kutoka mkoa wa Mbeya na Songwe kutokana na hofu ya kukabiliana na presha ya wananchi ni jambo liloratibiwa,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema kuwa bado wanaimani na mahakama lakini hawakuwa na imani ya Hakimu aliyetoa hukumu ile kutokana na alionekana akiendesha kesi kwa kupokea maagizo ambapo ni kinyume na weledi wa taaluma hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!