Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe ahitimisha siku 226 mahabusu
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe ahitimisha siku 226 mahabusu

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Aikaeli Mbowe leo Ijumaa, tarehe 4 Machi 2022 amehitimisha siku 226 za kuwa mahabausu kwa tuhuma za ugaidi. Anaripoti Rhoda Kanuti, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe alikamatwa usiku wa tarehe 21 Julai 2021 jijini Mwanza, saa chache kabla ya kuongoza kongamano lililokuwa limeandaliwa na vijana wa Chadema (Bavicha) la kudai Katiba Mpya.

Mara baada ya kukamatwa, alisafirishwa hadi jijini Dar es Salaam na Jeshi la Polisi kisha kuunganishwa katika kesi ya ugaidi na watuhumiwa wengine watatu, Adam Kasekwa, Halfan Bwire na Mohame Ling’wenya.

Watuhumiwa hao watatu, walikuwa makondamoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikosi 92KJ cha Ngerengere mkoani Morogoro ambao wao walimatwa mwaka 2020.

Soma zaidi:-

Mbowe aliyewahi kuwa mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro pamoja na wenzake, walikuwa wakituhumiwa kwa mashtaka matano ya kupanga njama za kufanya ugaidi katika maeneo mbalimbali nchini.

Watuhumiwa hao wote walikutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam mbele ya Jaji Joachim Tiganga aliyekuwa anaisikiliza kesi hiyo.

Tiganga alikuwa Jaji wa tatu kuisikiliza mahakamani hapo, tangu ilipoanza Septemba 2021 akitanguliwa na Elinaza Luvanda aliyeombwa na kina Mbowe ajitoe naye akakubali kisha akafutia Mustapha Siyani ambaye yeye ajitangaza kujitoa baada ya kuwa ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Jaji Kiongozi.

Ikiwa leo Ijumaa tarehe 4 Machi 2022 ndiyo siku ambayo Mbowe na wenzake walikuwa wanatakiwa kuanza kujitetea, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Mwandamizi, Robert Kidando ameieleza mahakama kwamba, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kwa matinki hiyo, Jaji Tiganga amewaachia huru bila masharti Mbowe na wenzake ambao hata hivyo hawakuwepo mahakamani hapo.

Jambo hilo liliibua shangwe ndani na nje ya viwanja vya mahakama hiyo, iliyopo Mawasiliano kwa wanachama kushangilia na kuimba nyimba mbalimbali pamoja na mawakili wa utetezi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!