April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe aeleza siri ya Dk. Mahanga Chadema

Mwili wa Dk. Milton Makongoro Mahanga ukiwa katika taratibu za mwisho nyumbani kwake Segerea, Dar es Salaam kabla ya kwenda kuzikwa

Spread the love

MOJA ya jambo kubwa na la kipekee kwa marehemu Dk. Makongoro Mahanga, ni kuwa mtu wa kujifunga na kutokuwa na haya katika kubadilika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni kauli ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), iliyowakilishwa na John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho wakati akisoma salamu zake za rambirambi, kwa familia ya marehemu Dk. Mahanga leo tarehe 26 Machi 202.

Kwenye ujumbe huo, Mbowe amesema Dk. Mahanga ameacha somo zito katika chama hicho kufuatia utayari wake katika kukubali kujirekebisha bila kuwaonea aibu wengine.

“Dk. Mahanga atadumu kuwa somo muhimu kwa chama chetu tunapoelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa 2020. Tusihukumu kwa jumla, bali kila mmoja kwa hulka na karama zake tena kwa pande zote.

“Walio ndani ya chama tayari na hata walio vyama vingine. Watu hubadilika, wakati wote tujifunze, wakati wote tusione haya kujirekebisha kwani hakuna mazingira yadumuyo ndani ya siasa,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema, Dk. Mahanga nzi za uhai wake alionesha msimamo wake katika kukataa kuwa mamluki, kutokana na kitendo chake cha kukwepa kushirikiana na kundi aliloliita mamluki ,lililoibuka katika Uchaguzi wa Mkuu wa Chadema.

“Alipendwa sana na wengi ndani ya chama. Aliponzwa kwa kiasi fulani wakati wa uchaguzi mkuu ndani ya chama na doa jeusi, lililopakwa na wengine waliohamia upinzani toka CCM waliokosa msimamo pale maslahi yao binafsi yalipohatarishwa,” amesema Mbowe na kuongeza;.

“Chama chetu kilijaribiwa na kundi hili na wanachama wakakilinda chama chao kwa wivu mkubwa. Dk. Mahanga akawa mhanga wa hofu hiyo alipojaribu kugombea nafasi katika ngazi ya taifa, kwenye Baraza la Wazee. Bado, hakuyumba.”

Katika salamu zake hizo zilizosomwa na Mnyika, Mbowe ameeleza zaidi kwamba, Dk. Mahanga hakuwa mroho wa madaraka, na alivumilia mitihani aliyoipata kutokana na hatua yake ya kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Aliendelea kusimama na chama kwa nafasi ya mkoa na kuendelea kuwa kielelezo chema kwamba si sahihi kuhukumu kila atokaye CCM au Vyama vingine kuwa ni mamluki au msaka madaraka au mdhambi.

“Alijipambanua kukipigania chama chake si kwa wivu tu, bali pia kwa umakini mkubwa zaidi hadi umauti ulipomkuta,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Nina hakika, pamoja na kudumu Chadema kwa kipindi cha miaka minne na miezi tisa tu, ubora wake uliweza kujipambanua barabara. Mnyenyekevu lakini asiyeyumba kimsimamo hata fimbo za Maisha, watawala na dola zilipobana.”

error: Content is protected !!