Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe abanwa kizimbani, apangua hoja
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe abanwa kizimbani, apangua hoja

Spread the love

FREEMAN Mbowe Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kuwa ametoa maelezo polisi juu ya kutoweka kwa msaidizi wake Ben Saanane. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akihojiwa na upande wa Jamhuri leo Tarehe 8 Novemba 2019, baada ya kumaliza kuwasilisha utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Jopo la Mawakili watano wa serikali lililongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Faraja Nchimbi, Joseph Pande, Wankyo Simon, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Jackline Nyantori na Salim Msemo.

Huku upande wa utetezi  uliongozwa na Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya.

Yafuatayo ni mahojiano ya Mbowe na mawakili wa serikali juu ushahidi aliouwasilisha mahakamani hapo.

Jackline: Shahidi umeieleza mahakama kuwa uchaguzi uligubikwa na matatizo mengi ikiwa pamoja na mawakala wenu kuziwa mpaka kupelekea kufungua kesi ulisema kesi namba ngapi?

Mbowe: Kesi namba 129 ya mwaka 2018.

Jackline: Mahakama gani ?

Mbowe: Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam.

Jackline: Kwa ujumla shtaka liliishaje?

Mbowe: Liliondolewa mahakamani.

Jackline: Ni sahihi kwamba mlihitimisha kampeni zenu kwenye viwanja vya Buibui?

Mbowe: Ni sahihi.

Jackline:Ni sahihi kwamba katika hadhara ile kulikuwa na watu mbalimbali walikuwepo wenye elimu wa darasa la saba na walikuwa hawana elimu kabisa?

Mbowe: Sina uhakika.

Jackline: Kabla hamjaanza mkutano mlichukuwa rekodi ya  kujua wamehudhuria watu fulani fulani?

Mbowe: Hapana.

Jackline:  Wakati unatoa ushahidi wako ulieleza mlikutana na watu mbalimbali kwenye makutano ya barabara ya Kawawa na Mwananyamala na wewe ulikuwepo?

Mbowe: Ndio.

Jackline: Hapo na Buibui kuna umbali gani?

Mbowe: Kama mita 50.

Jackline: Ni sahihi kwamba Akwelina alifariki kwenye barabara hiyo ya Kawawa.

Mbowe: Ndio nilivyosikia.

Jackline: Mheshimiwa Mbowe kama nimekusikia vizuri unadai

Hakimu: Shahidi.

Jackline: Shahidi kama nimekusikia vizuri umezungumzia kwenye ushahidi wako kwamba mara ya kwanza Gerald Ngichi umemuona wapi?

Mbowe: Hapa mahakamani.

Jackline: Mbali na Ngichi, shahidi gani mwingine wa Jamhuri uliyepata kuonana naye?

Mbowe: Hakuna.

Jackline: Ni sahihi kuwa kwenye uchaguzi wa Kinondoni hapakuwa na mgombea anayeitwa Magufuli?

Mbowe: Sahihi.

Baada ya kumaliza kumhoji wakili Jackline alimkabidhi kijiti wakili Pande na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:-

Pande: Shahidi kwa kusikiliza elimu yako uliyonayo hakuna ubishi kiswahili unakifahamu vizuri?

Mbowe: Sahihi.

Pande: Kuna wakati wowote uliwahi kupata tatizo la kumbukumbu?

Mbowe: Bado.

Pande: Kuna wakati wowote uliwahi kupata tatizo la akili?

Mbowe: Bado.

Pande: Nilikusikia ukisema wewe ni mkristo na kusema uongo ni dhambi?

Mbowe: Sahihi.

Pande: Siku ya tarehe 16 Februali, 2018 pale Buibui Ground kulikuwa na watu wengi walijaza kiwanja utakubaliana na mimi kuwa ili watu wote wakusikie ulitumia spika?

Mbowe: Sahihi.

Pande: Utakubaliana na mimi kuwa pale Buibui Ground kuna ukaribu na barabara ya Mwananyamala  kabla ya lami kuna njia ya vumbi sawasawa?

Mbowe: Sawa.

Pande: Kwa uelewa wangu kutoka Buibui hadi barabara ya Mwananyamala takribani viwanja viwili au vitatu vya mpira.

Mbowe: Sijui.

Pande: Kwa ufahamu wako ni viwanja vingapi?

Mbowe: Mita hamsini.

Pande: Utakubaliana na mimi makutano ya barabara ya mwananyamala ni viwanja vitano vya mpira?

Mbowe: Siyo kweli

Pande: Kiasi gani?

Mbowe: Mita arobaini.

Pande: Na Buibui mpaka barabara ya Mwananyamala?

Mbowe: Mita kumi

Pande: Kwa mujibu wa shtaka la nne kina nani ambao waliumizwa?

Mbowe: Shtaka la nne hatukuandaa sisi kwa hiyo sijui.

Pande: Shtaka la nne ulisomewa?

Mbowe: Ndio.

Pande: Kina nani waliumizwa?

Mbowe: PC Fikiri na Koplo Rahim Msangi.

Pande: Utakubaliana na mimi ukitoka makutano ya barabara ya Kawawa na Mwananyamala utapita Mkwajuni kisha ndio utafika katika ofisi za halmashauri ya Kinondoni?

Mbowe: Kwa mtu anayepita njia hiyo ni sawa.

Pande: Ulivyohojiwa na Wakili Nyantori ulisema ulipata taarifa Jamii Forum?

Mbowe: Miongoni mwa source.

Pande: Jamii Forum ni site ambayo mtu anachapisha anachojisikia sawasawa?

Mbowe: Jamii forum ni chanzo chenye ukweli.

Pande: Ulichosikia Jamii Forum kilithibitishwa?

Mbowe: Naomba nijibu kwa urefu mheshimiwa hakimu.

Pande: Mimi nataka kwa ufupi…Jamii Forum ni chombo cha uchunguzi?

Mbowe: Sio cha uchunguzi lakini taarifa nyingi za kweli.

Pande: Ulieleza hukuwepo kwenye matukio yote hukushuhudia?

Mbowe: Sikushuhudia nilisikia.

Pande: Namaanisha matukio ya kuuawa kwa Alfonce Mawazo, Daudi Mwangosi, kushambuliwa Lissu na kupotea Ben Saanane kuna tukio lolote ulilolitaja ulikwenda Polisi kuandika maelezo?

Mbowe: Ndio tukio la Ben Sanane.

Pande: Hayo mengine yote hukuyaandikia maelezo polisi ni sahihi?

Mbowe: Sahihi kabisa.

Pande: Katika maelezo yako polisi ulimtaja mtu yoyote aliyehusika?

Mbowe: Sikumbuki

Wakati huo huo Wakili Pande alimkabidhi kijiti Wakili Nchimbi aliyemuomba Hakimu Simba ahairishe kwa kuwa yeye atahitaji kielelezo namba 5 (P5) ambacho ni (Min Div) video.

Shauri hilo litaendelea wiki ijayo tarehe 13, 14 na 15 Novemba, mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

error: Content is protected !!