SERIKALI ya kaunti ya Vihiga nchini Kenya imezindua mradi ambao utasaidia kutengeneza mbolea ya bei nafuu inayotokana na kinyesi cha binadamu ili kuwapunguzia wakulima makali ya bei yam bole ya viwandani katika uimarishaji wa kilimo kwenye eneo hilo.
Katika kutekeleza mradi huo, tayari Serikali ya nchi hiyo imejenga Kituo cha kuhifadhi kinyesi katika mji wa Mbale, kilichogharimu Sh milioni 324. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Kituo hicho kitakuwa kinakusanya kinyesi cha binadamu huku kikitoa magari sita yakubebea kinyesi hicho.
Mkurugenzi wa usafi wa mazingira katika kaunti ya Vihiga, James Odiero alisema mbolea kutoka kwenye kinyesi cha binadamu itauzwa kwa wakulima kati ya Ksh 300 hadi 500 sawa na Tsh 5,714 hadi 9,522 kwa mfuko mmoja.
Odiero alisema mradi huu ambao ulianza mwaka wa 2020 na kuchukua miaka miwili kukamilika.
“Kupitia mradi huu, tutasafisha kinyesi kutoka kwenye vyoo na kisha kukitengeneza kuwa mbolea ambayo itauzwa kwa wakulima.
“Hili litarudishia faida zilizotumika kujenga mradi huo. Kila siku tutasafisha cubu 50 za kinyesi hicho ambayo ni sawa na lita 50,000 za takataka zilizotolewa na mashine sita za exhauster,” alifafanua.
Gavana Wilber Ottichilo alisema mpango huo utaimarisha kilimo na pia utasaidia kuhamasisha jamii zilizokuwa zinakwepa kujenga vyoo.
“Mradi huu utasaidia kusafisha mazingira yetu na kuziba uharibifu wa kila namna wa mazingira,” Ottichilo alisema.
Leave a comment