
Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema. Picha ndogo Rais John Magufuli
UAMUZI mdogo kuhusiana na kesi ya “dikteta uchwara” inayomkabili Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu unatarajiwa kutolewa Oktoba 4, mwaka huu, anaandika Hellen Sisya.
Mahakama ya Hakimu Mkazai Kisutu ya jijini Dar es Salaam, inatarajiwa kutoa uamuzi huo baada ya kupokea na kupitia utetezi wa maandishi wa Lissu na upande wa Jamhuri.
Kwa mujibu wa mahakama hiyo utetezi wao unatakiwa kuwasilishwa ndani ya siku 14 kuanzia leo.
Katika kesi hiyo ambayo inasikilizwa na hakimu, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mwanasheria huyo anawakilishwa na Wakili Peter Kibatala, huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na wakili Mutalemwa Kishenyi.
Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), anashtakiwa kwa madai kuwa alimwita Rais John Magufuli dikteta uchwara.
Anadaiwa kutamka maneno hayo akiwa katika mahakama hiyo miezi kadhaa iliyopita.
Mwanasheria huyo anadaiwa kuwa alitoa kauli hiyo wakati anatoka katika kesi nyingine iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na madai ya uchochezi katika gazeti la Mawio.
More Stories
Bawacha yasitisha kongamano la siku ya wanawake duniani
Rais Mwinyi amwapisha mrithi wa Maalim Seif
Mrithi wa Maalim Seif aahidi haya