May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbivu, mbichi ripoti BoT wiki hii

Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Spread the love

 

RIPOTI ya ukaguzi wa matumizi ya fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa mwezi Januari mpaka Machi mwaka huu, kuwekwa hadharani wiki hii. Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam…(endelea).

Kuali hiyo imetolewa na Rais Samia Suluhu Hassam leo tarehe 28 Juni 2021, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam.

Rais Samia ametoa maelezo hayo baada ya Mhariri wa Clouds Media ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA), kutaka kujua hatua iliyofikiwa kuhusu ripoti hiyo.

Joyce She, Mhariri wa Habari, kituo cha Radio Clouds FM

“Nadhani swali limewahi, Jumanne nina kikao na NEC (Kamati Kuu ya CCM), Jumatano ama Alhamis napokea ripoti hizo na umma utajua kilichomo,” amesema Rais Samia.

Wakati akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru Ikulu ya Chamwino, Dodoma tarehe 28 Machi 2021, Rais Samia aliagiza kufanyika uchunguzi ili kubaini matumizi ya fedha hizo.

Rais Samia alitoa maagizo hayo alipozungungumzia upotevu wa fedha huku akimuelekeza CAG na Takukuru kwenda kupekua fedha zilizotolewa BoT katika kipindi hicho.

“…lakini upotevu mkubwa unatokea huko, na wewe mwenyewe CAG umesema hali si shwari na hatua za haraka zinahitajika.

“Naomba nitoe agizo kwako na Takukuru, naomba nenda pitia na Gavana wa benki yupo hapa, pitieni fedha zote zilizotoka katika kipindi cha Januari mpaka Machi mwaka huu, zilizokwenda kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo tunataka kuziona,” alisema Rais Samia.

error: Content is protected !!