Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbivu, mbichi kesi ya kina Mdee kujulikana leo
Habari za SiasaTangulizi

Mbivu, mbichi kesi ya kina Mdee kujulikana leo

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, inatarajia kutoa uamuzi dhidi ya maombi yaliyofunguliwa na wabunge viti maalum 19, wakiongozwa na Halima Mdee, ya kuomba kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama cha Chadema. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa leo Jumatano, tarehe 6 Julai 2022, kuanzia saa 6.00 mchana, mahakamani hapo mbele ya Jaji Mustafa Ismail.

Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi kama inatoa kibali cha kufunguliwa kesi hiyo ya kina Mdee kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, au la.

Tarehe ya kutolewa uamuzi huo ilipangwa na Jaji Ismail, wiki iliyopita baada ya Mdee na wenzake 18, kuwasilisha hoja tano, wakiiomba mahakama ifanye mapitio ya kimahakama, juu ya mchakato uliotumika kuwafukuza uanachama wa Chadema.

Mawakili wa kina Mdee walidai, mchakato huo ulikuwa kinyume cha sheria.

Wakili wa Chadema, wakiongozwa na Peter Kibatala (katikati) wakiwa mahakamani

Miongoni mwa hoja hizo tano ni, maombi ya kuomba mapitio hayo yalifunguliwa ndani ya muda kisheria, wabunge hao kuwa na maslahi dhidi ya mchakato huo wakidai uliwaathiri kufuatia hatua ya Chadema kuwavua uanachama.

Nyingine ni mchakato huo kuingiliwa na upendeleo kufuatia ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, waliowafukuza uanachama, kushiriki kikao cha Baraza Kuu la Chadema, kilichotupilia mbali rufaa zao za kupinga kufukuzwa.

Hoja nyingine ni maamuzi ya Chadema kuwafukuza uanachama kuwa ya umma na mwisho ikiwa wabunge hao kukosa nafasi ya kupata haki yao ya kusikilizwa juu ya uamuzi huo.

Mbali na Chadema iliyoshtakiwa kupitia Bodi yake ya Wadhamini, wajibu maombi wengine katika shauri hilo ni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!