September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbeya City yaididimiza Coastal, Mwadui hoi nyumbani

Spread the love

HALI ya Coastal Union imedizi kuwa mbaya baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Mbeya City katika mchezo uliocheza kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Mbeya City iliwachukua dakika tano kupata bao la kwanza lililofungwa na Salvatory Nkulula bao lililodumu mpaka mapumziko.

Wakati Coastal wakijiuliza kipindi cha pili wapate bao la kusawazisha, lakini Nkulula aliipatia Mbeya City bao la pili dakika ya 50, bao la tatu lilifungwa na Hassan Mwasapili, kabla ya Ditram Nchimbi kukwamisha la mwisho.

Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa leo, timu ya Mwadui FC imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kujikuta wanapoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mwadui Complex.

Wakati huohuo timu ya Taifa ya Vijana ya chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeibuka kidedea katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Vijana ya Misri kwa ushindi wa mabao 2-1, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Serengeti yamefungwa na Cyprian Benedictor dakika 15 na Ally Hussein dakika ya 89 wakati bao la Misri limefungwa na Wahed dakika 86.

error: Content is protected !!