July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbeya City yafufukia Msimbazi, yaichapa 2-1

Mashabiki wa timu ya Mbaye City wakishangilia baada ya mechi hiyo kwisha na kuibuka na ushindi

Spread the love

TIMU ya Mbeya City ambayo ilionekana kuanza vibaya msimu huu, leo imefufua matumaini yake katika mchezo wake dhidi ya Simba baada ua kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, mechi iliyopchezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, anaripoti Erasto Stanslaus.

Mbeya City ambayo msimu uliopita ilikuwa moto wa kuotea mbali na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya nne, kabla ya mchezo wake na Simba ilikuwa katika nafasi ya tatu kutoka mkiani.

Lawama za Simba zitamwangukia beki mkongwe, Nassor Masoud baada ya kukosa penalti dakika ya mwisho huku timu yake ikiwa imelala kwa mabao 2-1. Penalti ya Cholo iligonga mwamba wa juu dakika ya 90+3 baada ya beki Yussuf Abdallah kumchezea rafu kiungo Jonas Mkude kwenye boksi.

Wakati Chollo anakosa penalti hiyo, wenzao waliitendea haki mkwaju wa penalti walioupata dakika ya 90+2 iliyokwamishwa wavuni ya Yussuf Abdallah baada ya kipa Peter Manyika kumshika miguu Raphael Daudi.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambua wa Shinyanga aliyesaidiwa na Anold Bugado wa Singida na Yahya Ali wa Mara, hadi mapumziko tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Bao la Simba lilifungwa na mshambuliaji chipukizi, Ibrahim Salum Hajib kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20, baada ya kiungo Awadh Juma kuchezewa rafu.

Mbeya City ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Hamad Kibopile dakika ya 77 akitumia vizuri makosa ya mabeki wa Simba SC kuchanganyana na kipa wao, Peter Manyika.

Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Simba SC katika Ligi Kuu chini ya kocha mpya, Mserbia Goran Kopunovic aliyeshinda mechi moja 2-0 dhidi ya Ndanda na baadaye sare ya 1-1 Azam FC.

error: Content is protected !!