Saturday , 22 June 2024
Home Kitengo Michezo Mbeya City yaendelea kupata tabu Ligi Kuu
Michezo

Mbeya City yaendelea kupata tabu Ligi Kuu

Spread the love

TIMU ya Mbeya City imeendelea kupata tabu katika Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kupoteza mchezo wa tatu mfululizo dhidi ya Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mbeya City ilianza kwa kichapo katika mchezo wao dhidi ya Simba mabao 2-0 kabla kupigwa tena idadi kama hiyo na klabu ya Azam FC. 

Mabao ya Mtibwa katika mchezo wa leo yalifungwa na Stamili Mbonde katika dakika ya tisa, Ismail Mhesa 42 na bao pekee la kufutia machozi kwa Mbeya City lilifungwa na Eric Kyaruzi.

Kwa matokeo hayo Mbeya City itakuwa imeruhusu jumla ya mabao sita mpaka sasa katika michezo mitatu iliyocheza na kuendelea kuburuza mkia katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara na kufanya kuwa na mwanzo mbaya.

Licha ya kutokuwa na nyota wao wawili muhimu wa kikosi cha kwanza Kelvin Sabato na Salum Kihimbwa ambao wapo kwenye majukumu ya timu ya Taifa, Mtibwa ilionekana kucheza vizuri na kumiliki mpira muda wote wa mchezo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ukiwa na Meridianbet ni kula pesa tu

Spread the love  Alhamisi ya leo mechi za EURO zinazidi kuendelea huku...

Michezo

Leo pesa utaipatia kwa Ureno na Uturuki ukiwa na Meridianbet

Spread the love  Kama kawaida michuano ya EURO 2024 inazidi kupamba moto...

Michezo

Leo Uingereza, Uholanzi zote kukupa pesa

Spread the love Siku ya leo EURO 2024 kupigwa katika viwanja mbalimbali,...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

error: Content is protected !!