January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbatia: Ukawa tupo imara

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia

Spread the love

JAMES Mbatia-Mwenyekiti mwenza wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), amesema hakuna mgogoro wowote kati ya vyama vya NCCR – Mageuzi na Chama cha Demokrasia na Maendele (Chadema).  Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Ukawa inaudwa na vyama vya Chadema, NCCR – Mageuzi, CUF na NLD.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mbatia aliye pia Mwenyekiti wa NCCR–Mageuzi, amesema “kuna baadhi ya vyombo vya habari vinapotosha na kudai ndani ua Ukawa kuna migogoro.”

“Aliyetoa taarifa hizo kwenye magazeti sio kiongozi ndani ya Ukawa wala chama chochote cha siasa. Sisi ndani ya Ukawa hatuna mgogoro,” amesema Mbatia.

Aidha, Mbatia ameeleza kuwa Ukawa wanajitahidi kupunguza migogoro ndani ya jamii na kuzungumza namna ya kuongoza taifa kwa kuwa na rais mmoja na mbunge mmoja ambapo kwa sasa wapo katika hatua nzuri.

Amesema mgogoro batili unaotajwa na vyombo vya habari ni kuhusu chama chake kugombana na Chadema kuhusu nafasi ya urais, umakamu wa rais na uwaziri mkuu.

“Hizo chokochoko zinazoendelea kwenye magazeti eti Ukawa yasambaratika, NCCR wagombana na Chadema; sio sahihi, ni taarifa potofu. Tupo imara kwa maslahi ya mama yetu Tanzania. Hatutaki kuwa sehemu ya migogoro ya nchi hii ya wafanyakazi, walimu, wazee na wabunge,” amesisitiza Mbatia.

error: Content is protected !!