Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbatia atoa wosia kwa Watanzania kuelekea 28 Oktoba
Habari za Siasa

Mbatia atoa wosia kwa Watanzania kuelekea 28 Oktoba

Spread the love

JAMES Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi nchini Tanzania, amewataka Watanzania kutumia kura zao vizuri katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, ili kuamua mustakabali mwema wa maisha yao katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbatia ametoa wito huo leo Alhamisi tarehe 10 Septemba 2020 katika uzinduzi wa kampeni za NCCR-Mageuzi katika Jimbo la Kinondoni, zilizofanyika Kata ya Ndugumbi-Magomeni Dar es Salaam.

Mgombea wa Jimbo hilo kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi ni Mustafa Muro, ambaye alinadiwa na Mbatia kwenye uzinduzi huo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mbatia amesema, kura ya Mtanzania katika uchaguzi huu ina thamani kubwa kuliko kipindi chochote, kwa kuchagua viongozi sahihi watakaoleta muafaka wa kitaifa pamoja na maendeleo ya nchi na Watanzania kwa ujumla.

“Kwa hiyo, WanaKinondoni na Watanzania kwa ujumla, kwa kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni uchaguzi wa kuamua hatma ya maisha yetu kwa miaka mitano ijayo, kuamua maisha yetu yatakua ya namna gani? Kura yako thamani yake ni ya msingi kwa maisha ya binadamu,” amehasa Mbatia.

Wakati huo huo, Mbatia amesema, chama chake hakitatumia kampeni za uchaguzi huo zinazoendelea hivi sasa kutusi au kugombana na watu bali kitazungumzia sera zitakazoleta afya kwa Tanzania.

“Nawaomba tuchuje pumba ni ipi, vipo vyama vya siasa kazi yao kutukana lakini sisi  NCCR tunazungumzia utu wa binadamu, kulieta taifa pamoja, tunazungumzia namna gani kuifanya mama Tanzania anenepe vizuri anyoshe watoto wake. sisi hatuhitaji kusema watu, kugombana na watu wala kutukana watu tunahitaju,” ameeleza Mbatia.

Mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi amesema ambaye pia ni mgombea ubunge wa Vunjo Mkoa wa Kilimanjaro amesema, chama hicho kimejipanga kuwaletea Watanzania viongozi watakaotatua shida zao sambamba na kurudisha furaha katika maisha yao.

“Wanasema midomo inaumba, Watanzania tunakosa majawabu kwamba kesho yetu inakuaje sababu hawana furaha wana wasiwasi.”

“Uchaguzi huu, tuutumie kubadilisha maisha yetu na hili halichagui chama, kote kuna wasiwasi na takwimu za dunia zinazoonyesha tumeshika nafasi mbaya kwa kukosa furaha kwa sababu afya zetu hazituruhusu kuwa na furaha,” amesema

“Hatuishi katika misingi ya kula vizuri na kulala vizuri. Tunahishi kwa msongo wa mawazo ili haya tuondokane nayo inabidi tufikirie  tunapata kiongozi wa aina gani,” amesema Mbatia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!