Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Maisha Afya Mbatia ataka vituo chanjo ya Korona viongezwe
Afya

Mbatia ataka vituo chanjo ya Korona viongezwe

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameiomba Serikali iongeze vituo vya kutolea huduma ya chanjo ya Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbatia ametoa wito huo leo Jumanne, tarehe 3 Agosti 2021, baada ya kuchanjwa chanjo ya Korona, Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi, ameishauri Serikali iruhusu vituo vya afya vya watu binafsi vitoe huduma hiyo, ili chanjo ziwafikie kwa urahisi wananchi hasa wa vijijini.

“Serikali yetu iachane na urasimu iruhusu sekta binafsi nayo iwekeze vya kutosha, kuhakikisha watu wanatoa huduma hii. Mfano Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (Ilala), ina vituo nane vya kuchanja. Kigamboni wana vituo vitano mpaka sita kwa wilaya nzima. Watu watachanjwa namna gani?” amesema Mbatia.

Mbatia ameongeza “ukiangalia mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi ambayo ina majimbo mawili ya uchaguzi ina vituo vitatu tu. Jimbo la Vunjo lenye vijiji zaidi ya 78, lina kituo kimoja. Manispaa ya Moshi ina vituo vinne tu, miundombinu ya kutoa huduma hii iko chini sana.”

Mwanasiasa huyo ameiomba Serikali iongeze nguvu katika utoaji huduma ya chanjo, ili kukabiliana na ugonjwa huo unaoathiri uchumi wa dunia.

“Serikali iweke kipaumbele namba moja kwenye hili, Serikali ikiwekeza vya kutosha kwenye jambo hili inakuza uchumi wake,” amesema Mbatia.
Pia, Mbatia ameiomba Serikali iongeze nguvu katika kuwapa elimu wananchi, juu ya umuhimu wa chanjo hiyo.

Serikali ya Tanzania imeanza kutoa huduma hiyo leo Jumanne, baada ya zoezi la uchanjaji kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, tarehe 28 Julai mwaka huu, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Mbatia amewaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kupata chanjo ya Korona.

“Rais yangu kwa Watanzania wote tukubali kuchanjwa, kwani kutokubali kuchanjwa ni kuwa gizani. Kuchanjwa ni kwenda kwenye nuru, kufanya jambo jema na kuwa na usalama kuliko usumbufu wa aina yoyote,” amesema Mbatia.

Takribani vituo 550 vimepangwa na Serikali, kwa ajili ya kutolea huduma ya chanjo ya Korona Tanzania Bara.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali ya Tanzania kupokea dozi 1,058,400, za chanjo hiyo aina ya Johnson & Johnson kutoka kwa Serikali ya Marekani, kupitia mpango wake wa Covax, unaolenga kusaidia nchi zinazoendelea katika kukabiliana na janga hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Waziri wa Tamisemi apewa siku 14 afike Morogoro kutatua changamoto za Afya

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel...

Afya

Ma-RMO, DMO watakiwa kujitafakari ubadhirifu hospitali za mikoa, wilaya

Spread the love  NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amewataka waganga...

Afya

JK atoa ya moyoni kuhusu huduma za afya

Spread the love  RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amesema huduma za afya...

AfyaHabari za Siasa

Heche amvaa Ummy Mwalimu kisa bima ya afya

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche amemtaka...

error: Content is protected !!