Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbatia ampinga Rais Magufuli
Habari za Siasa

Mbatia ampinga Rais Magufuli

Spread the love

MSIMAMO wa Rais John Magufuli, kwamba hatosaidia watakaokumbwa na mafuriko, umepingwa na James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mbatia ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Februari 2020, mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Tarehe 11 Februari 2020, wakati akizindua wilaya mpya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alisema, serikali haitatoa msaada wa aina yoyote kwa watu waliojenga mabondeni, sababu wameyataka wenyewe.

“Hakuna cha kusaidiwa, uliyatafuta mwenyewe hayo mabonde ngoja yakubondoe ili ujifunze mwenyewe…,” alisisitiza Rais Magufuli.

 Hata hivyo, Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo, ameishauri serikali na Watanzania, kusaidia wahanga wa mafuriko, badala ya kuwalaumu.

“Tushirikiane kuhakikisha tunawatia moyo na tunawasaidia. Katika suala hili hatunyoosheani vidole, tunakuja pamoja tunatatua tatizo ndio tunakuja kulaumiana baada ya kushughulikia kwa pamoja.

“Lazima kushikamana kwa pamoja. Tutoe rai, inapotokea mambo kama haya, tuwe pamoja. Kwa kweli tukiwa pamoja tutashinda. Kutiana moyo kutafakari kwa pamoja, tukitumia taasisi zetu mbalimbali hili suala halifungamani na itikadi za siasa au dini,” amesema Mbatia.

Pia mwansiasa huyo ameshauri serikali kuanzisha chombo maalumu kitakachoshughulikia masuala ya majanga nchini, ili kupambana na kudhibiti maafa yatokanayo na majanga mbalimbali.

“Je, tulijua litatokea lini? Na tutapambana nalo vipi au ni janga ambalo hatujui litatokea lini? Tujiulize, tumejiweka tayari kwa kiasi gani kuwa tayari kupambana na kujikinga na majanga.

“Tunayo sheria ya 2015, ambayo tulijitahidi kushauri kushawishi namna bora ya kupambana na majanga na kujiandaa kukabiliana nayo,” amesema Mbatia.

Amefafanua, kwamba sheria inasema kuwe na mamlaka kamili ya kusimamia majanga, “…lakini hiyo mamlaka mpaka sasa hivi haijaanzishwa kwa mujibu wa sheria ya 2015.”

Amesema “sheria itekelezwe ili tuweze tukawa na mamlaka rasmi kwa mujibu wa sheria ili tuweze kusimamia janga.”

Hata hivyo, Rais Magufuli alisema, watu wengi hujenga katika sehemu zenye mikondo ya maji hasa mabondeni, wakati wakijua kwamba kuna uwezekano wa kupatwa na mafuriko.

Kiongozi huyo wa nchi alishauri watu waliko katika maeneo yanayoweza kukumbwa na mafuriko, kuchukua tahadhari ya kuondoka katika maeneo hayo, ili wasiathirike na mafuriko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!