January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbatia ahimiza ushirikiano vita dhidi ya UVIKO-19

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amewaomba Watanzania washirikiane katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbatia ametoa wito huo leo Alhamisi, tarehe 2 Desemba 2021 akizungumza na wanahabari, mkoani Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi, amewaomba Watanzania washirikiane katika kinga dhidi ya ugonjwa huo, pamoja na kujiandaa dhidi ya wimbi la nne la ugonjwa huo linalodaiwa kuibuka katika mataifa ya Kusini mwa Afrika.

“Sisi NCCR tunaomba ushirikiano wa Watanzania wote, ushirikiano wa dunia katika hayo mambo makuu matatu tuliyosema, ya kinga na kuwa tayari wakati wowote, preventation (kudhibiti) preparedness (utayari) and respond,” amesema Mbatia.

Mwanasiasa huyo amesema“Tanzania kila wiki tungetoa takwimu wangapi wamechanjwa.”

Mbatia ametoa wito kwa viongozi wa Serikali, kuongeza juhudi katika kutafuta tiba dhidi ya janga hilo, ikiwemo kufuata ushauri wa watalaamu wa afya.

“ Tusingependa tu afariki dunia sababu ya janga hili, wakati tuna hekima na uwezo, viongozi wafuate ushahuri wa watalamu. Tujiulize Watanzania ni asilimia ngapi tumeshachanja?,”amesema Mbatia na kuongeza:

“Na viongozi wengine wanazunguzma kwenye majukwaa wanazungumzia UVIKO-19 hawajachanjwa, mimi nazungumzia hili sababu nilichanja hadharani na familia yangu yote kuonesha kuwa kiongozi ni kuwa kielelezo katika jamii.”

error: Content is protected !!