
Wataalam wa BVR wakiweka sawa mashine hiyo kabla ya kuanza kuandikisha wapiga kura
DAKTA Antony Mbassa – aliye mbunge wa Biharamulo (Chadema), ameitaka Serikali ieleze kwanini uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura umekuwa na mizengwe na kusababisha wananchi kukata tamaa. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Dk. Mbassa ametoa kauli hiyo wakati akiomba mwongozi kwa lengo la kutaka kujua hatima ya uandikishwaji katika daftari hilo ambao unaonekana kujawa na mizenge katika maeneo mbalimbali.
Amesema kwa sasa katika maeneo mbalimbali wananchi wamekuwa wakitishiwa na watendaji kwa kufukuzwa huku baadhi ya vifaa vya BVR vikihamishwa bila kujali kuwa wananchi hawajajiandikisha.
Mbali na hilo alitaka kujua kama serikali ina mpango wa kuongeza muda wa uhandikishwaji kutokana na uliotengwa kutotosha huku changamoto zikiwa ni nyingi.
Akitoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), Jenister Mhagama, amesema kuwa amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wabunge mbalimbali.
Hata hivyo, amesema kuwa si vyema watendaji wakawanyanyasa wananchi na kuwafanya washindwe kujiandikisha katika daftari hilo na kwamba serikali inaendelea kufanyia kazi chamgamoto ambazo zimekuwa zikilalamikiwa.
More Stories
Sensa ya watu na makazi Tanzania ni zaidi ya kuhesabiwa
Mambo yanayombeba Rais Samia kimataifa
Waziri Mkuu Uingereza aponea kung’olewa