December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbarouk amhakikishia ushirikiano Balozi DRC

Spread the love

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amepokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) nchini, Jean-Pierre Massala katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara tarehe 15 Novemba, 2022 Jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza baada ya kupokea nakala hizo, Balozi Mbarouk amemhakikishia Balozi huyo kuwa Serikali itampa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini.

Balozi Mbarouk ameongeza kuwa Tanzania na DRC zitaendelea kushirikiana kwenye masuala mbalimbali yenye maslahi kwa pande zote mbili hususan biashara na uwekezaji.

error: Content is protected !!