December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbaroni kwa kumlawiti mama yake mzazi

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto

Spread the love

KIJANA mmoja ambaye hakutajwa jina, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kumlawiti mama yake mzazi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa hiyo imethibitishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Dodoma, Giless Muroto wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 4 Julai 2019.

Kamanda Muroto amesema, mtuhumiwa anadaiwa kumlawiti mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 56 kwa kumvizia.

Amesema, chanzo cha mtuhumiwa huyo kumlawiti mama yake, kinaweza kuwa ni ulevi au imani za kishirikina.

Wakati huo huo, Kamanda Muroto amesema, Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa wengine wawili kwa makosa ya ulawiti na ubakaji wa watoto na wazee.

Aidha, Kamanda Mroto amesema mtu mmoja ameuawa na wananchi wenye hasira kali, akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa miaka nane.

error: Content is protected !!