Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mbaroni kwa kumkata mkono albino
Habari Mchanganyiko

Mbaroni kwa kumkata mkono albino

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Urlich Matei
Spread the love

JESHI la polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumkata mkono mlemavu wa ngozi /albino katika kijiji cha Nyarutanga kata ya Kisaki wilaya ya Morogoro Vijijini, anaandika Christina Haule.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro (ASP) Leonce Rwegasira, amesema kuwa tukio la kwanza lilitokea Oktoba 3 saa 6 usiku katika kijiji cha Nyarutanga ambapo watu wasiojulikana walivamia nyumba ya Nassoro Msingili (75) mkazi wa kijiji ambaye ni mlemavu wa ngozi/albino na kumkata mkono wa kushoto.

Kamanda huyo amesema kuwa Msingili akiwa amelala ndani ya nyumba yake alivamiwa na watu hao wasiojulikana na kisha kumkata mkono wake wa kushoto na kukimbia nao kusikojulikana.

Amesema majeruhi huyo amelazwa katika kituo cha afya Duthumi akiendelea kupatiwa maibabu huku yake ikizidi kuimarika.

Hata hivyo amesema juhudi za kuwatafuta waliofanya uhalifu huo zinaendelea ambapo tayari watu wawili ambao hakutaja majina yao kufuatia kuendelea kufanya uchunguzi ili kubaini watu wote waliohusika katika tukio hilo.

Aidha amesema jeshi hilo linapinga vikali mauaji na ukatili unaofanywa kwa albino na linaendeleza msako mkali kuwasaka wale wote wanaojihusisha na matukio kama hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!