January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbaroni kwa kughushi majina ya CCM, M4C

Spread the love

WATU watatu wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa kwa makosa manne ya kutumia vibaya mtandao ili kujipatia fedha isivyo halali huku wakitumia jina la Chama cha Mapinduzi (CCM) na Movement For Change. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Akiwasomea mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Kalegeya Abeisiza, Mwendesha mashtaka wa Serikali, Castus Ndamugoba, alidai washitaki wote kwa pamoja walikula njama ya kughushi majina ya vyama vya siasa kinyume na sheria 384 kifungu namba 16.

Kosa la pili ni la Oktoba 2 la kujaza fomu ya kufungua akaunti katika benki ya NMB na kuambatanisha na fomu yenye barua ya kughushi ya CCM iliyotambulika kwa jina la CCM Spridon Dini.

Hata hivyo kosa la tatu ni watuhumiwa wote kughushi barua ilionekana imesainiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kosa la nne ni kuomba fedha Sh. 4 millioni kutoka kwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina moja la Omega.

Kesi hiyo namba 158 ya mwaka 2015, watuhumiwa hao wanatuhumiwa kufanya makosa hayo kati ya Septemba na Oktoba mwaka huu jijini hapa kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia zisizokuwa halali.

Mdamugoba amesema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walishirikiana kufungua akaunti katika benki ya NMB tawi la Mwanza lililopo katika barabara ya Kenyata mjini hapa kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kwamba akaunti iliyokutwa na kiasi cha fedha Sh. 4 millioni ilikuwa na majina ya Movement for Change na ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambako waliwadanganya wananchi na wafanyabiashara kwamba kuchangia kampeni za vyama hivyo.

Watuhumiwa hao ambao ni Boni Bukulu (mkazi wa Mahina), Spriodon Njunwa (Igoma) na Braiton Wilson (Bugando) wote wakiwa ni wakazi jijini hapa.

Hata hivyo kesi hiyo imehailishwa hadi Novemba 30 mwaka huu na watuhumiwa wamerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana.

error: Content is protected !!