Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbarawa akagua barabara VETA-Uhasibu, atoa darasa kwa madereva
Habari Mchanganyiko

Mbarawa akagua barabara VETA-Uhasibu, atoa darasa kwa madereva

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila (katikati), alipokagua na kuruhusu kuanza kutumika kwa njia moja katika barabara ya Juu Chang'ombe Jijini Dar es Salaam leo ili kupunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Nyerere.
Spread the love

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewataka madereva kutumia barabara ya juu ya Veta Chang’ombe na Uhasibu kwa kufuata sheria za usalama barabarani ili iweze kudumu kwa muda mrefu. Anaripoti Selemani Msuya … (endelea).

Prof. Mbarawa ameyasema hayo leo tarehe 30 Mei, 2022 wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo ambayo upande mmoja wa magari yanayotoka Gongo la Mboto na ile inayotoka Mbagala eneo la Uhasibu kukamilika kwa asilimia kubwa, hivyo inaruhusiwa kutumika kupunguza msongamano.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuruhusu kuanza kutumika kwa njia moja katika barabara ya Juu Chang’ombe Jijini Dar es Salaam leo ili kupunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Nyerere.

Amesema kazi iliyobakia katika barabara hizo ambazo zimeruhusiwa ni ndogo, hivyo kitaalam zinaruhusiwa kutumia, ila kinachotakiwa ni madereva kufuata sheria za barabarani katika matumizi yake.

“Msongamano Dar es Salaam ni mkubwa, hivyo hakuna sababu ya kuacha barabara ambayo ipo tayari ikae kusubiri kipande kingine, hii sio sawa naomba kipande hiki kianze kutumika baadae tutafunga kuweka lami nyepesi na taa kazi ambayo inaweza kufanyika kwa siku moja au mbili,” amesema.

Mbarawa amesema mkandarasi wa miradi hiyo barabara za juu na mwendokasi bado yupo ndani ya mkataba, hivyo ni matumaini vipande vilivyobakia vitakuwa vimekamilika ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kumkomboa Mtanzania kwa kila sekta, hivyo ujenzi wa barabara za juu, maradaja ni moja ya eneo ambalo litasaidia kufikia malengo hayo.

Waziri huyo amewataka askari wa usalama barabarani kuendelea kusimamia na kuongoza magari kwa kufuata sheria na taratibu za nchi.

Aidha, Waziri Mbarawa amewataka madereva kutumia barabara kwa uangalifu ili kutokwamisha miradi inayoendelea kujengwa ikiwemo Daraja la Kamata ambalo linajengwa.

Prof.Mbarawa amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inamaliza msongamano wa mafari katika jiji la Dar es Salaam ikiwa ni kukamilisha ujenzi wa barabara za juu na mwendokasi.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania, Mhandisi Rogatus Mativila amesema ujenzi wa barabara hiyo ya juu umezingatia viwango vya kimataifa ambapo ina uwezo wa kupitisha magari hadi yenye uzito wa tani 56 na kuendelea.

“Hii barabara ina viwango vya barabara kuu, ambapo gari yenye uzito wa tani 56 inaruhusiwa kupita bila tatizo lolote. Matarajio yetu ni ifikapo Machi 2023 ujenzi huu wa BRT II itakuwa imekamilika na kupunguza msongomano,” amesema.

Mhandisi Mativila amesema ujenzi wa barabara hizo ni awamu ya pili ya BRT na kwamba bado awamu zingine nne ambazo zikimalizika msongamono jijini Dar es Salaam utakuwa umepungua kama sio kuisha kabisa.

Amesema mradi wa BRT awamu ya pili unagharimu zaidi y ash.bilioni 200, hivyo kuwataka Watanzania kutumia barabara hizo kwa uangalifu.

Naye Mkuu wa Kikosi ya Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdi Isango amesema kufunguliwa kwa barabara hizo mbili za Veta Chang’ombe na Uhasibu kutapunguza foleni kwa asilimia kubwa.

“Maeneo haya ajali ndogo ndogo zinatokea na sababu ni madareva kugombania kupita, hivyo kufunguliwa kwa barabara hii kutapunguza ajali. Lakini pia mafuta hayatatumika kwa wingi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!