March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbao FC waitoa nishai Gor Mahia

Spread the love

KLABU ya Mbao FC imefanikiwa kuiondoa timu ya FC Gor Mahia kutoka Kenya kwenye michuano ya kombe la Sport Pesa kwa njia ya mikwaji ya penalti 4-3 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo hivyo nakufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Gor Mahia ambao walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo kwa miaka miwili mfululizo ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Oriech dakika ya  56, na baadae Mbao wakafanikiwa kusawazisha dakika ya 76 kupitia Aboubakar Ngalema.

Baada ya ushindi huo Mbao FC  itakutana na Kariobang Sharks kutoka Kenya katika mchezo wa nusu fainali siku ya Ijumaa.

Ikumbukwe bingwa wa michuano hiyo atapata zawadi ya kombe na kiasi cha fedha Sh. 30 milioni sambamba na kucheza mechi na klabu ya Evarton FC inayoshiliki Ligi Kuu nchini England mwezi Julai mwaka huu.

error: Content is protected !!