April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mazishi ya usiku yamshtua Zitto

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo

Spread the love

WAKATI Serikali ya Tanzania ikipiga marufuku utaratibu hasi wa mazishi ya usiku katika Halmashauri kadhaa nchini, Zitto Kabwe ameitaka serikali kutimiza wajibu wake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini amesema, kwa sasa inashuhudiwa misiba mingi na watu kuzikwa usiku.

“Sitaki kuhisi kuna kitu kinafichwa. Nataka serikali itimize wajibu wake… Hivi sasa tuna shuhudia misiba mingi, mazishi ya watu usiku usiku na hata miili ya watu mitaani,” Zitto ameliambia Shirika la Habari la BBC.

Hata hivyo, serikali imepiga marufuku mazishi ya usiku, ikieleza watu wanaofariki kwa ugonjwa wa corona ama vinginevyo, wapewe heshima inayostahili.

“Katika kipindi hiki, tunaelekeza maofisa afya na waganga wakuu wa wilaya na mikoa, kuhakikisha familia zinashirikishwa kikamilifu na bila hofu au haraka katika kuandaa na kufanya mazishi kwa heshima zote za utu,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Profesa Abel Makubi, Mganga Mkuu wa Serikali.

Kauli ya namna hiyo imewahi kutolewa na Job Ndugai, Spika wa Bunge kwamba, ni haki marehemu kuzikwa sehemu ambayo amilia yake imependa.

error: Content is protected !!