May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mazishi ya TB Joshua kufanyika siku 7

Spread the love

 

MWILI wa aliyekuwa Muasisi wa Kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN), Temitope Balogun Joshua ‘TB Joshua’ (57), unatarajiwa kuzikwa Jumapili tarehe 11 Juni 2021, katika viwanja vya kanisa hilo, Jijini Lagos nchini Nigeria. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Mwili huo unazikwa ikiwa ni mwezi mmoja, tangu Mhubiri huyo mashuhuri nchini Nigeria, alipofariki dunia tarehe 5 Juni 2021.

Kwa mujibu taarifa ya kanisa hilo, shughuli za mazishi ya mwili wa TB Joshua zitafanyika kwa muda wa siku saba, kuanzia leo Jumatatu, tarehe 5 hadi 11 Julai 2021.

Shughuli hizo zitatanguliwa na ibada ya kuwasha mishumaa, itakayofanyika katika Kanisa la SCOAN, jioni ya leo.

Waumini wa kanisa hilo wameagizwa kwenda na mishumaa yao katika ibada hiyo, kwa ajili ya kuiwasha ikiwa ni heshima ya mwisho kwa mhubiri huyo.

Ibada hiyo ya kuwasha mishumaa itarushwa moja kwa moja, katika kituo cha televisheni cha kanisa hilo, Emmanuel TV.

Jumanne ya tarehe 6 Julai 2021, itafanyika ibada ya kutoa heshima za mwisho kwa viongozi wa SCOAN, kisha kufuatiwa na ibada ya kusifu na kuabudu usiku kucha hadi kuamkia Jumatano, tarehe 7 Julai 2021.

Alhamisi ya tarehe 8 Julai 2021, wafuasi na wananchi wengine wa TB Joshua watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho.

Ijumaa ya tarehe 9 Julai 2021, SCOAN itaweka za video za kuonesha kumbukumubu za mahubiri na mafunzo ya TB Joshua.

Mazishi ya TB Joshua yanatarajiwa kuwa ya faragha Jumapili ya tarehe 11 Julai mwaka huu.

Kamishna wa Afya wa Jiji la Lagos,Prof. Akin Abayomi, amesema wataalamu wa afya watatumwa katika siku hizo za mazishi, kuhakikisha hatua za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19), zinachukuliwa.

error: Content is protected !!